Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake, Job Ndugai akichukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
Ndugai ambaye amekuwa katika nafasi hiyo katika Bunge la 11 amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha leo katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu kwa Katibu Msaidizi Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda, Ndugai amewaomba Watanzania wamuombee ili chama kimteue katika nafasi hiyo.
Aidha Itunda amesema kuwa fomu hizo zinatolewa kwa gharama ya Sh 500, 000 na zoezi hili litafikia kikomo leo saa 10 jioni.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇