NAM: USHINDI WA MAGUFULI UTAIFANYA TANZANIA IJIKOMBOE KIUCHUMI
Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) umempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ushindi wa kishindo huku ukisema kwamba ushindi huo utaiwezesha Tanzania kujikomboa kiuchumi kwa kuendeleza harakati za kuwa Taifa linalojitegemea.
Katika ujumbe huo wa kumpongeza Rais Dkt. Magufuli uliotolewa na Mwenyekiti wa NAM Mhe. Ilham Aliyev, umoja huo unasema ushindi wa kishindo alioupata Rais Magufuli unaonesha jinsi watanzania
wanavyounga mkono sera ya ujamaa na kujitegemea.
“Tunampongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ushindi wa kishindo, ushindi alioupata unaonesha watanzania wanataka kujitegemea, tuna imani kwamba miaka mitano ijayo Tanzania itapiga hatua kubwa ya maendeleo” alisema
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇