LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 1, 2020

DK MAGUFULI KUAPISHWA ALHAMISI NOVEMBA 5, MWAKA HUU



 Na Richard Mwaikenda, Dodoma.

RAIS Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ambaye leo amekabidhiwa na NEC cheti cha uchindi, anatarajiwa kuapishwa kushika rasmi wadhifa huo katika sherehe zitakazofanyika Alhamis Novemba 5 kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Dk Magufuli ambaye aligombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi,CCM, ameshinda ushindi wa kimbunga kwa kupata zaidi ya kura milioni 12 ambazo ni sawa na zaidi ya asilimia 84.


Katika sherehe hizo pia ataapishwa aliyekuwa Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Mteule wa Zanzibar aliyegombea kupitia CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuapishwa kesho Unguja Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages