Na Allawwi Kaboyo.
Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi Mkoani Kagera, Mhandisi Ezra John Chiwelesa, ameapa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kufa na kupona, ikiwa ni kutimiza ndoto zake za kuleta maendeleo ambayo wananchi waliomuamini wamekuwa wakitamani kuyaona kwa kipindi kirefu.
Akizungumza nje ya Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, baada ya kula kiapo hicho Mhandisi Ezra John Chiwelesa ammesema kuwa ubunge alioupata sio wake bali ni imaani kubwa aliyopewa na wananchi wa Biharamulo hivyo anawajibika kuwatumikia kwa kutekeleza ahadi alizozitoa pamoja nakuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichompa dhamana ya kugombea.
Mhandisi Ezra amesema Halmashauri ya Biharamulo haina sababu ya kuwa miongoni mwa Halmashauri za mwisho kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhesabiwa kwenye Halmashauri ambazo wananchi wake ni masikini wakati vipo vyanzo vingi vya mapato kwenye wilaya hiyo.
Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha pili cha serikali ya awamu ya tano watajitahidi kuwa na Baraza bora la Madiwa ambalo litasimama kwa ajili ya kuwatetea wananchi pamoja na kusimamia mapato ii kuweza kukuza uchumi wa wanabiharamulo ambapo ameongeza kuwa atatuia muda mwingi jimboni kufanya kazi za wananchi pale atapokuwa hana vikao vya bunge.
Akizungumzia ahadi yake ya kumuajili mwanasheria kwaajili ya kutoa msaada wa kisheria, Mhandisi Ezra amesema kuwa ahadi hiyo ipo pale pale na atahakikisha wananchi wenye matatizo ya kisheria wanapata msaada huo bila kulipia.
Katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia, Hamashauri ya wiaya Biharamulo Chama Cha Mapinduzi kimefanikiwa kupata madiwani wote kwa kata 17, huku mbunge wa jimbo hilo akishinda kwa zaidi ya asilimia 70.
Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhandisi Ezra John Chiwelesa akila kiapo cha kuwa mbunge wa jimbo hilo, wakati wa uapisho wa wabunge, Bungeni jijini Dodoma, jana.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇