LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 11, 2020

CHRISANT MZINDAKAYA ATAKA CCM ISIBWETEKE NA USHINDI MKUBWA ILIOUPATA KATIKA UCHAGUZI MKUU ULIOFANYIKA HIVI KARIBUNI

Mwanasiasa mkongwe Mzee Crisant Mzindakaya akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally alipofika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, leo.


Na Mwandishi Maalum, Dom
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally amepokea salam za pongezi kwa niaba ya CCM kutoka kwa mwanasiasa mkongwe nchini na mbunge mstaafu Mzee Crisant Mzindakaya.


Katibu Mkuu amepokea pongezi hizo, leo tarehe 11 Novemba, 2020 Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma alipotembelewa na kufanya mazungumzo na Mzee Crisant Mzindakaya.


"Nimeona nifike hapa Makao Makuu ya Chama, niweze kuwapongeza viongozi wetu, kwanza nianze na Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye ni Katibu Mkuu. Dkt. Bashiru ni mtu mwenye historia nzuri katika wataalam waliobobea kwenye mambo ya siasa na kubobea kwake kwenye mambo ya siasa kumeleta matunda." 


Akisisitiza, Mzindakaya ameeleza kuwa, Uchaguzi wa mwaka huu wa chama ulikuwa umepangwa vizuri na mafanikio yamekuwa mazuri na ni yeye Katibu Mkuu ndio aliongoza shughuli hiyo ingawa aliwatumia na watu wengine ikiwemo na mimi mwenyewe.


Aidha Mzindakaya, ameeleza umahiri na Uchapakazi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwa ndio kigezo kingine kikubwa kilichosababisha ushindi mkubwa na wa kihistoria katika Uchaguzi uliyopita.


Wakati huo huo, Mzindakaya ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa viongozi wote kutobweteka na ushindi huu mkubwa, wafanye tathmini na waongeze uwajibikaji zaidi kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi ujao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages