LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 20, 2020

Video & Picha: KATIBU UWT DODOMA MJINI MADUKWA AONGOZA KUZISAKA KURA ZA DK MAGUFULI SOKO KUU LA MAJENGO DODOMA

KATIBU wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara wakiwa na picha za kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli alipowaongoza wajumbe wa Kamati Maalumu ya Ushindi ya UWT, kuzitafuta kura za wagombea wa CCM katika Soko Kuu la Majengo Dodoma leo Oktoba 20, 2020..
Mjumbe wa Kamati Maalumu ya Ushindi, Khadija Hamsini akimuonesha picha ya Dk. Magufuli mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu la Majengo kwa lengo la kumuomba .
Baadhi ya Mama lishe na wateja wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Maalumu ya UWT ya Ushindi, Flora Liacho aliyekuwa akifanya kampeni za kuwaombea kura wagomea wa CCM.
Mama mfanyabiashara ndogo ndogo nje ya Soko la Majengo, akipokea picha ya Dk. Magufuli kutoka kwa Mjumbe wa Kamati Maalumu ya Ushindi, Joyce Smacus.
 

Na Richard Mwaikenda, Dodoma.


KATIBU wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana leo amewaongoza wajumbe wa Kamati ya Ushindi kuzitafuta kura za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na Mgombea Udiwani Kata ya Majengo, Shifaa Ibrahim katika Soko Kuu la Majengo jijini hapa.


Diana ambaye aliongozana na Khadija Hamsini, Flora Liacho na Smacus walilishambulia soko hilo kila kona wakielezea sera nzuri za CCM pamoja na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mgombea wa CCM, Dk Magufuli.


Wengi wa wafanyabiashara walionekana kufurahishwa na mtindo huo wa kuwathamini kwa kufuatwa maeneo yao ya biashara hivyo kupata fursa pia ya kuelezea kero zao ili wazifikishe ngazi ya juu kwa wahusika kwa lengo la kupata ufumbuzi.


Tukio lingine lililoonesha kuwa Dk. Magufuli anapendwa ni picha zake za kampeni walizokwa wanazigawa wajumbe wa kamati ya ushindi, kugombewa na kila mfanyabiashara sokoni hapo hadi zikaisha huku wakisema kura za Magufuli hazina mjadala watampigia mapema Oktoba 28, 2020. Pia waliahidi kuwapigia Mgombea Ubunge Dodoma Mjini na madiwani katika Kata wanazoishi.


Asilimia kubwa ya wafanyabiahara walionekana  kuwa na imani kubwa na Rais Dk Magufuli hasa kutokana na uchapakazi wake kiasi kwamba hawakusita kuelezea maendeleo makubwa aliyoifanyia Tanzania na Dodoma kwa ujumla.


Walitaja baadhi kuwa ni: Dodoma kutangazwa kuwa Jiji, kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma, Rais kuhamia Ikulu ya Chamwino, Ujenzi wa Stendi ya Kisasa na Soko la Kisasa la Job Ndugai.


Miradi mingine ni;Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR, kuanza kwa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na kuanza ujenzi wa barabara za pete (Ringroads) kulizunguka jiji la Dodoma na hivi karibuni JPM ametangaza kujenga Uwanja Mkubwa wa Kisasa wa michezo.


Lakini pia baadhi ya akina mama waliokutwa wakifanya biashara ndogo ndogo nje ya soko hilo, walimwambia Katibu wa UWT, Diana kuwa Rais Magufuli amewatoa kwenye mateso ya kila mara kufukuzwa na mgambo wa Manispaa na kuporwa bidhaa zao, lakini yeye alipoingia madarakani amewaruhusu kufanya biashara bila matatizo, hivyo hawana kingine cha kumlipa zaidi ya siku hiyo kwenda kumpigia kura nyingi za ndio.


"Magufuli ametuokoa kutoka kwenye manyanyaso makubwa tuliyokuwa tunafanyiwa na Mgambo wa Manispaa, waliokuwa wanatufukuza na kunyang'anya bidhaa zetu tulizokuwa tunauza nje ya soko hili, lakini baada ya yeye kuingia madarakani ametutetea tunafanya biashara bila bugudha, kweli katuvisha nguo, nasi hatuna cha kumlipa zaidi ya kumpigia kura nyingi za ndiyo," alisema Habiba Haji huku kauli hiyo ikiungwa mkono na wenzie Rehema Sambali na Mwantumu Abdalla.


Diana na wajumbe wa kamati hiyo ya ushindi walifanya kampeni sokoni hapo kwa kuwatembelea akina mama lishe,  wauza mazao mbalimbali, wauza kuku, wauza mbogamboga na matunda, bucha, waendesha bodaboda, Bajaji, washonaji nguo na wauzaji wa bidhaa za aina mbalimbali.


Kwa uhondo zaidi tazama tukio hilo kuitia clip hii ya video...

 

 

 Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages