Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Korogwe kwenye uwanja wa TTC mkoani Tanga kabla ya kuelekea Same mkoani Kilimanjaro kuendelea na mikutano ya kapeni leo Jumanne Oktoba 20,2020.
Rais Dk John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika Mkutano huo amewaasa vijana kutoshiriki maandamano yeyote yanayohamasishwa na baadhi ya wagombea ili kulinda amani ya nchi kama ilivyoachwa na muasisi wa taifa hili Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
(PICHA NA JOHN BUKUKU -KOROGWE)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Korogwe kwenye uwanja wa TTC mkoani Tanga kabla ya kuelekea Same mkoani Kilimanjaro kuendelea na mikutano ya kapeni leo Jumanne Oktoba 20,2020.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu akiwa pamoja na baadhi ya wagombea ubunge wa mkoa wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa TTC Korogwe.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu akimkaribisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuzunguza na wananchi wa Korogwe mkoani Tanga katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu TTC.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili kwenye uwanja wa TTC mjini Korogwe kwa ajili yakuhutubia mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu wakati alipowasili kwenye uwanja wa TTC mjini Korogwe kwa ajili yakuhutubia mkutano wa kampeni
Mgombea Ubunge wa jimbo la Muheza Mwana FA akizungumza kuhusu mambo mbalimbali yaliyofanyika katika jimbo hilo na serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Mbunge mteule wa jimbo la Pangani Ndugu Jumaa Aweso akizungumza maendeleo yaliyofanyika kwenye jimbo lake.
Mbunge mteule wa jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akimuombea kura Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa TTC mjini Korogwe.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole akitoa ratiba ya mkutano huo.
Sheik Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakary Zubeir akisoma dua katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa TTC mjini Korogwe.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli akimvisha kofia msanii Kassim Mganga.
Mgombea ubunge wa jimbo la Tanga mjini Ndugu Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa TTC mjini Korogwe
Mgombea Ubunge wa jimbo la Muheza M Khamisi Mwinyjuma Mwana FA na Mausa Sama wakiimba jukwaani katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe.
Dula Makabila akitumbuiza kwenye mkutano huo.
Msanii Kassim Mganga akifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe mkoani Tanga leo.
Baadhi ya picha zikionesha maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇