LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 17, 2020

UTIAJI SAINI HATI ZA MAKUBALIANO KUONDOA HOJA ZA MUUNGANO WAFANYIKA LEO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar Mhe. Issa Haji Gafu wakitia saini Hati za makubaliano ya kuondoa Hoja 5 za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi ikiwemo ushirikishwaji wa SMZ kwenye masuala ya Kimataifa na Kikanda, Hafla iliyoshudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhun Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  iliyofanyika leo Octoba 17,2020 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Biashara Viwanda na Uwekezaji Mhe. Inocent Bachungwa kushoto na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali wakibadilishana  Hati za makubaliano ya kuondoa Baadhi ya Hoja za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi kuhusu Biashara muda mfupi baada ya kusaini Hati hizo katika Hafla iliyoshudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhun Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo Octoba 17,2020 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Bara Dkt. Alan Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee wakibadilishana  Hati za makubaliano ya kuondoa Hoja za Muungano zilizopatiwa ufumbuzi kuhusu uandaaji Vikao vya pamoja  muda mfupi baada ya kusaini Hati hizo katika Hafla iliyoshudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhun Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo Octoba 17,2020 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihitubia Taifa kwa njia ya Televisheni na Redio kwenye  kikao cha Utiaji saini Hati za makubaliano ya kuondoa Hoja za Muungano  zilizopatiwa ufumbuzi, ambapo Hoja 5 zimeondolewa ikiwemo ushirikishwaji wa SMZ kwenye masuala ya Kimataifa na Kikanda na Biashara, Hafla hiyo  imefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akilihitubia Taifa kwa njia ya Televisheni na Redio kwenye  kikao cha Utiaji saini Hati za makubaliano ya kuondoa Hoja za Muungano  zilizopatiwa ufumbuzi, ambapo Hoja 5 zimeondolewa ikiwemo ushirikishwaji wa SMZ kwenye masuala ya Kimataifa na Kikanda na Biashara, Hafla hiyo  imefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages