LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 17, 2020

DK. BASHIRU AZINDUA MAFUNZO YA MAWAKALA WA CCM MWANZA, ASEMA MAJIMBO YOTE MKOANI HUMO YATABAKIA CCM

Na Mwandishi Maalum, Mwanza

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally amezindua mafunzo ya mawakala wa CCM katika Uchaguzi Mkuu mkoa wa Mwanza na kueleza kuwa, mafunzo hayo sasa yanaendelea nchi nzima.


Uzinduzi huo ulifanyika jana, Ijumaa,Oktoba 16, 2020 katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.


"Nimeamua kuja Mwanza kufanya kazi ya kuzindua mafunzo kwa viongozi wa Chama na mawakala wa uchaguzi kwa niaba ya Chama kwa sababu za kimkakati, Kwanza, tumeshakubaliana na Mwenyekiti wa Mkoa kwamba hakuna jimbo lolote la mkoa huu litakalotoka mikononi mwa CCM ", alisema Dk. Bashiru


Baadaye Katibu Mkuu, alishiriki ibada ya Ijumaa katika msikiti wa Mkoa wa Mwanza, ambapo alitumia fursa hiyo kutoa shukrani kutoka kwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, kwa viongozi wa dini zote nchini kuendelea kuhimiza amani na mshikamano bila kuchoka wakati wote hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi Mkuu hadi siku ya uchaguzi mkuu wenyewe utakaofanyika siku ya Jumatano, Oktoba 28, mwaka huu na pia baada ya uchaguzi huo.


Said Said Nguya ambaye ni Afisa Habari katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM amesema Dk. Bashiru ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mwanza , atakuwa mkoani hapa katika ziara hiyo ambayo ni ya siku nne na leo alitarajiwa kuwa katika Wilaya ya Nyamagana.  

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akipokewa na Vijana wa CCM alipowasili kwenye viwanja vya Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza jana.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza alipowasili jana. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Anthony Diallo.
Ukifanywa utambulisho
Gari alilomo Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally likiingia Uwanja wa CCM Kirumba
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Mwanza wakati akienda eneo la tukio baada ya kufika katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza wakati akizindua 
mafunzo ya mawakala wa CCM katika mkoa wa Mwanza kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika siku ya Jumatano, Oktoba 28, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages