Baadhi ya Viongozi wa dini ,Wawakilishi wa vyama vya siasa,Wazee wa Mila waliomba Dua kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28.
viongozi wa dini wakifuatilia mjadala katika kongamano la Amani lililofanyika mkoani Arusha
……………………………………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi Wetu -Arusha
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa itahakikisha Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28,2020 inakuwa huru na wa haki.
Pia Nec imesema kuwa itahakikisha kuwa vifaa vyote vinavyohusika na Uchaguzi mkuu vinafika kwa Wakati katika maeneo yote nchini.
Akizungumza kwa njia ya simu katika kongamano la Amani lililoandaliwa na taasisi ya dini ya kiislamu ya Twariqa Tanzania lililofanyika mkoani Arusha, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi dkt.Wilson Charles Mahera alisema kuwa time hiyo itahakikisha kuwa changamoto zote zinatatuliwa.
“Kwanza niwapongeze viongozi wa dini kwa kuweza kukutana hapo Arusha nilitamani niwe pamoja nanyi lakini majukum ya kikazi Sasa nipo Songea Ila napenda kuwafahamisha Watanzania kuwa Uchaguzi mkuu utakuwa huru na wa haki,pia tume ya Taifa kwa kushirikiana na watu wangu tutahakikisha kuwa maandalizi yote yanakamilika kwa wakati na vifaa vyote vitafika kwa Wakati”alisema dkt.Mahera
Aidha aliwatoa hofu Watanzania kuwa hakuna sheria ya Uchaguzi itakayokiukwa bali sheria na taratibu zote zitafuatwa ikiwa ni pamoja na Mgombea atakayeshinda atatangazwa.
“Ndugu zangu viongozi wa dini hakuna sheria itakayobadilika bali tutafuata sheria na taratibu zote zilizopo na kuhakikisha kuwa Uchaguzi unakuwa huru na wa haki kikubwa wagombea wawahimize wafuasi wao kwenda kupiga kura,na kutanguliza amani Kama kauli mbiu yenu inavyosema “Tanzia kwanza,Kuna Maisha baada ya Uachaguzi”alisema dkt.Mahera
Naye katibu mkuu wa Taasisi ya Twariqa Tanzania Shekhe Yahya Mkindi alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuendelea kuhubiri Amani na kukumbusha viongozi wa dini wajibu wao wa kuendelea kusisitiza Amani.
Mkindi alisema kuwa Hayati baba wa Taifa Mwl.Jukius Kambarage Nyerere akiwaachia Watanzania tunu kubwa ambayo ni Amani hivyo kuwataka Watanzania kuendelea kudumisha tunu hiyo.
Kwa kwa Upande wake msemaji wa Taasisi hiyo Shekhe Haruna Hussein aliwataka wanasiasaa kuhakikisha kuwa pamoja na Itikadi zao lakini bado wanajukum la kutanguliza maslahi ya Taifa mbele.
“Pamoja na kuwa katika kinyang’anyiro hiki kikubwa na kigumu lakini bado tuna wajibu wa kulinda Tanzania na kuhakikisha kuwa Maisha baada ya Uchaguzi yanaendelea Kama kawaida niwaombe Watanzania tuilinde Amani.”alisema Shekhe Haruna
Taasisi ya Twariqa Tanzania yenye makao yake mkoani Kilimanjaro imewakutanisha viongozi wa dini madhehebu mbali mbali, Viongozi wa Mila ya Kimasaai (Malaigwanani) na Viongozi wa Mila ya Meru (Washili ) mkoani Arusha lengo likiwa ni kuhubiri Amani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇