LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2020

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO OKTOBA 21, 2020


Mlinzi wa zamani wa Arsenal Per Mertesack anasema Mawazo ya Mesut Ozil yapo mbali mpira wa miguu
Maelezo ya picha,

Mlinzi wa zamani wa Arsenal Per Mertesack anasema Mawazo ya Mesut Ozil yapo mbali mpira wa miguu

Mlinzi wa zamani wa Arsenal Per Mertesacker anasema kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil mawazo yake yapo mbali mpira wa miguu - mchezaji huyo wa miaka 32 ameachwa kwenye kikosi cha Washika Bunduki cha Ligi Kuu ya siku ya Jumanne (Klick and Rush podcast via Mail)

Tottenham wapo mbioni kuingia mkataba mpya wa muda mrefu na mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min, 28. (The Athletic - subscription only)

Rio Ferdinand anaamini Ole Gunnar Solskjaer amesikitishwa na jinsi bodi ya timu hiyo ilivyoshindwa kufikia malengo yao
Maelezo ya picha,

Rio Ferdinand anaamini Ole Gunnar Solskjaer amesikitishwa na jinsi bodi ya timu hiyo ilivyoshindwa kufikia malengo yao

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini meneja Ole Gunnar Solskjaer amesikitishwa na jinsi bodi ya timu hiyo ilivyoshindwa kufikia malengo yao juu ya uhamisho kwenye dirisha la msimu wa joto. (BT Sport via Express)

Kiungo wa zamani wa Celtic na Rangers, Liam Burt, 21, alikuwa huko Pittodrie kwa pambano la Aberdeen la Premiership na Hamilton huku akienaendelea kutafuta nafasi kwenye vilabu vingine. (Daily Record)

Manchester City wako wazi kumpokea Pablo Zabaleta
Maelezo ya picha,

Manchester City wako wazi kumpokea Pablo Zabaleta

Manchester City wako wazi kumpokea Pablo Zabaleta anayerejea katika klabu hiyo kuchukua wadhifa ambao sio wa kimchezo kufuatia kustaafu kwa Muagentina huyo mwenye umri wa miaka 35-wiki iliyopita. (Mail)

Kocha wa Union Berlin Urs Fischer amekiri kwamba mlindalango wa Liverpool anayecheza kwa deni Loris Karius hakufurahi kwa kuachwa kwa benchi dhidi ya Schalke na anatumaini kuwa Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 27-ataonesha mchezo wake. (Inside Futbol)

Scott Duxbury amesema winga wa Senegal Ismaila Sarr, amejitolea kuisaidia klabu hiyo kurudi Ligi Kuu.
Maelezo ya picha,

Scott Duxbury amesema winga wa Senegal Ismaila Sarr, amejitolea kuisaidia klabu hiyo kurudi Ligi Kuu.

Mwenyekiti na mtendaji mkuu wa Watford, Scott Duxbury amesema winga wa Senegal Ismaila Sarr, 22, na mshambuliaji Muingereza Troy Deeney, 32, wamejitolea kuisaidia klabu hiyo kurudi Ligi Kuu. (London Standard)

Tafiti zinaonyesha makocha wa ligi kuu Uingereza wanadumu kwa muda mrefu zaidi katika ligi tano bora za Ulaya.(Mirror)

Ricardo Pereira,
Maelezo ya picha,

Ricardo Pereira, aliyefanyiwa upasuaji wa jeraha la goti anatumai kurejea Leicester City

Beki wa kulia wa Ureno, Ricardo Pereira, 27, aliyefanyiwa upasuaji wa jeraha la goti, anatumai atarudi kuichezea Leicester City ndani ya wiki sita. (O Jogo via The Independent)

AZ Alkmaar inasema wachezaji 13 wamebainika kuwa na virusi vya corona, lakini pambano lao la Ligi ya Uropa na Napoli siku ya Alhamisi bado litaendelea kama ilivyopangwa. (Mail)

Antoine Griezmann, 29, yupo tayari kupunguziwa sehemu ya mshahara wake.
Maelezo ya picha,

Antoine Griezmann, 29, yupo tayari kupunguziwa sehemu ya mshahara wake.

Mshambuliaji Mfaransa wa Barcelona Antoine Griezmann, 29, yupo tayari kupunguziwa sehemu ya mshahara wake. (Marca)

Liverpool wanamtaka difenda Muingereza anayechezea Brighton Ben White baada ya Leeds United kushindwa kusaini nae licha ya kwamba waliweka dau la kumnunua mara tatu kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 tu msimu huu. (Football Insider)

Cristiano Ronaldo amekosolewa
Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo amekosolewa

Waziri Vincenzo Spadafora amkosoa mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 35, kwa kurudi Italia kutoka Ureno baada ya kupimwa na kubainika ana maambukizi ya homa kali ya mapafu (COVID19). (Gazzetta dello Sport - in Italian)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages