LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 31, 2020

TRW:UCHAGUZI MKUU 2020 UMEZINGATIA KANUNI NA SHERIA


 
Mkurugenzi Mtendaji THE RIGHT WAY (TRW) Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu Mchakato wa Uchaguzi ulivyokwenda hivi karibuni.

Afisa Programu Uchaguzi na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Ibrahimu Samatta akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, kuhus mchakato wa Uchaguzi ulivyoenda.

……………………………………………………………………………………….
Taasisi ambayo ilikuwa inahusika na utoaji elimu ya Mpiga Kura na kutazama Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na kuhakikisha kuwa wa haki na usawa THE RIGHT WAY (TRW) wametoa mtazamo wao katika uchaguzi Mkuu na kueleza yakuwa Uchaguzi ulikuwa wa Haki na Usawa kwani wengi walifuata utaratibu uliowekwa bila kuvunja sheria.
TRW ilifanya utazamaji wa Uchaguzi Mkuu katika Mikoa 10 ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam,Tanga,Simiyu,Mwanza,Katavi,Geita,Kilimanjaro,Arusha,Dodoma,Mtwara na Mbeya.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu TRW Bw.Wallace Mayunga akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari Bw. Mayunga  amesema Uchaguzi umefanyika na washiriki wote wameepuka hali ya Rushwa na udanganyifu,kuna upatikanaji sawa wa rasilimali za taifa kwa wagombea wote wa vyama vyote vya siasa.

“Uchaguzi umefanyika katika mazingira ya amani na kwamba hakuna fujo wala vitisho, kuna fursa sawa za matumizi ya vyombo vya habari vya umma na binafsi kwa vyama vyote vya siasa pia kulikuwa na mazingira mazuri kwa wapiga kura kupata haki yao ya Kupiga kura hasa Tume imerahisisha kwa kuwepo kwa vituo vingi vya kupigia kura ili kila mmoja aweze kupata haki yake ya msingi”. Amesema Bw.Mayunga.

Aidha Bw,Mayunga amesema kuwa pamoja na changamoto za rasilimali fedha lakini wameweza kuifikia Mikoa 10 kwa kuweka watazanaji ambapo walifanya zoezi hilo na sasa wanaendelea kuwasilisha taarifa zao kwao ambazo zitasaidia katika kuandika taarifa yao kuu.

Pamoja na hayo Bw.Mayunga ametoa pongezi kwa jeshi la polisi na vyombo vya usalama kwani vimepiga hatua kuhakikisha usalama wa nchi na wapiga kura uliimarishwa kipindi chote cha Uchaguzi.



No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages