MABINGWA watetezi, Simba SC wamezinduka kutoka kwenye vipigo viwili mfululizo baada ya kuichapa 5-0 Mwadui FC Mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco katika dakika ya 25 na 64 ,Ajibu dakika ya 81,Hassan Dilunga dakika ya 87 na Said Ndemla dakika ya 90.
Huu ni ushindi wa kwanza katika mechi tatu, unaifanya Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck ifikishe pointi 16 baada ya kucheza mechi nane na kurejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Azam FC na Yanga wenye pointi 22 kila mmoja.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇