LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 30, 2020

WANAWAKE WAWILI KUTOKA CHADEMA NA CUF WASHINDA UBUNGE

 


Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Nkasi Kaskazini, amemtangaza Aida Khenani, wa CHADEMA kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo baada ya kupata kura 21,226, na kumshinda Ally Keissy wa CCM aliyepata kura 19,972 na hivyo yeye kuwa mgombea wa kwanza kukitetea chama chake katika nafasi hiyo.


Aida Khenani kabla ya Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa, alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 kupitia chama chake cha CHADEMA.


Mbali na CHADEMA kupata mtetezi wake wa kwanza Bungeni mpaka sasa tangu matokeo ya uchaguzi yaanze kutangazwa, chama cha CUF pia kinaye mwakilishi kutoka jimbo la Mtwara Vijijini, ambaye ni Shamsia Mtamba, aliyepata kura 26,262, na kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Hawa Ghasia aliyepata kura 18,505






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages