LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2020

PICHA ZA DK MAGUFULI ZAGEUKA LULU ZAGOMBEWA SOKO LA MAJENGO DODOMA

Mjumbe wa Kamati Maalumu ya Ushindi ya UWT CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Flora Liacho (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo Dodoma wakionesha picha za kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli huku wakiahidi kumpigia kura ili aongoze tena miaka mitano mingine. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
Katibu wa UWT CCM Wilaya ya Dodoma, Diana  Madukwa akiwa na waendesha bodaboda wakiwa mashika picha za Dk Magufuli katika Soko la Majengo.



Mjumbe wa  Kamati Maalumu ya Ushindi ya UWT, Khadija Hamsini (kulia), akimkabidhi stika ya picha ya Dk Magufuli mmoja wa wafanyabiashara sokoni hapo.

Diana  na mfanyabiashara wakionesha picha za Dk. Magufuli


Diana akimkabidhi picha ya kampeni ya Dk. Magufuli muuza dagaa
Bibi Khadija Salumu akipokea picha ya Dk. Magufuli kutoka kwa Khadija Hamsini wa UWT

Kija Masanja akiangalia picha ya Dk. Magufuli.
Wafanyabiashara wacheza  drafti wakiangalia picha ya Dk. Magufuli
Liacho wa UWT akimwaga sera na kuomba kura kwa akina Mama Lishe Sokoni hapo.
Wafanyabiashara wakiangalia picha ya kampeni ya Dk Magufuli
Mwanachama wa CCM anayeuza nazi sokoni hapo akionesha picha za Dk Magufuli.


Wanyabiashara wakibandika picha katika banda la mfanyabiashara ambaye amefunga ikidaiwa ameenda Mwanza kusaidia kampeni za Dk Magufuli ashinde.
Picha zikiwa zimebandikwa katika moja ya bucha zilizopo sokoni hapo.



 Akina mama wafanyabiashara ya matunda na mboga mboga sokoni hapo wakiwa na wajumbe wa Kamati ya Ushindi ya UWT wakionesha picha za Dk Magufuli. Akinamama hao walisema kuwa Dk Magufuli amewavisha nguo kwa kuwaruhusu kufanya biashara zao bila bughudha tofauti na awali walipokuwa wananyanyasika kwa kuporwa bidhaa zao na Mgambo wa Manispaa. Wameahidi kumpiga kura Oktoba 28.


Na Richard Mwaikenda, Dodoma.

PICHA na stika za kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli zimegeuka kuwa lulu kwa kugombewa na wafanyabiashara katika Soko Kuu la Majengo, jijini Dodoma juzi.


Picha hizo zilikuwa zinasambazwa na wajumbe wa Kamati Maalumu ya Ushindi ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, walioongozwa na Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo, Diana Madukwa. Wajumbe wengine ni Khadija Hamsini, Flora Liacho na Joyce Criacus pamoja na Mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo, Winfrida Kaliyo.


Kabla ya kuanza kuzigawa picha, wajumbe hao walikuwa wanaomba kura kwa kuelezea sera nzuri za CCM na mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ambaye ndiye mgombea urais kupitia chama hicho.


Walipokuwa wakielezea mafanikio aliyoyafanya Dk. Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, wengi wa wafanyabiashara na wateja walikuwa wakiwakatiza wasiendelee wakisema huyo haina haja kumuelezea kwani kila mmoja anajua ufanisi wake kinachosubiriwa ni kupigiwa kura Oktoba 28, 2020, bali wanachotaka wakati huo ni kupatiwa picha na stika  wabandike kwenye mabanda yao ya biashara.


"Aisee, usipoteze muda kuelezea kuhusu alichotufanyia Dk. Magufuli, kila mmoja anajua na mwenye macho anaona, we tupatie hizo picha tubandike kwenye vibanda vyetu, kura zake zinamsubiri Oktoba 28, lazima ashinde tu, hilo halina mjadala.


...Hivi kuna mtu asiyejua maendeleo mbalimbali aliyotufanyia Dk Magufuli? labda awe kipofu au kiziwi. Amejenga barabara lukuki za lami nchi nzima, amenunua ndege, anajenga chanzo kikubwa cha umeme Rufiji, Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR Dar -Dodoma unaendelea, ujenzi wa makao makuu ya nchi Dodoma, Soko Kuu la Job Ndugai, Stendi kubwa ya kisasa ya Dodoma na mambo mengine mengi," alimazia kusema Muuza nazi Hezron Chiposwa huku akiungwa mkono na baadhi ya wafanyabiashara wenzake.


Mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la  Sumbari, alisema kuwa ukitaka ukorofishane na watu sokoni hapo, ni kumsema vibaya Dk Magufuli, wanaweza kukupiga na hata kukuua, akidai kuwa huyo ni tunu tuliyopewa na Mungu, apigiwe kura aendelee kutuongoza.


Kabla ya kuyakaribia baadhi ya mabanda, wafanyabiashara wakawa wanatoka nje  na kuwafuata wajumbe walipo wapatiwe kwanza picha ya Dk. Magufuli halafu  ndiyo mambo mengine yafuate.


Kila mara picha na stika za Dk.Magufuli zilikuwa zinaisha mapema kwani hata wateja walikuwa wanazigombea, hivyo kuwafanya wajumbe kuhaha kwenda kuzichukua kwenye gari lakini hata hivyo zikawa hazitoshi kwa vile waliokuwa wanazihitaji walikuwa wengi.


Wajumbe walipata wakati mgumu, kuwaelezea wafanyabiashara sera za CCM, bila kuwa na picha za Dk Magufuli, maelewano yalikuwa hamna kwani wengi walikuwa wanazitaka picha zake kuliko maelezo huku wakisema haina haja kumuelezea Dk. Magufuli kila mmoja anajua alichokifanya ndani ya miaka mitano ya uongozi wake.


Baada ya kuona ugumu wa kuendelea kufanya kampeni bila picha za Dk Magufuli, Katibu wa UWT CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Madukwa alishauriana na wajumbe kuondoka na kuwaahidi wafanyabiashara waliokosa picha na stika kuwa watawapekelea siku inayofuata.Soko hilo linakadiriwa kuwa na zaidi ya wafanyabiashara 3000.


Wajumbe hao wa kamati maalumu ya ushindi ya UWT, walikwenda sokoni hapo kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM, Dk Magufuli anayegombea Urais, Anthony Mavunde anayegombea Ubunge Dodoma Mjini na Mgombea Udiwani wa  Kata ya Majengo lilipo soko, Shifaa Ibrahim.


Lakini licha ya kuomba kura kwa kumwaga sera za CCM na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, vilevile walikuwa wanasikiliza kero za wafanyabiashara hao kwa ahadi ya kuziwasilisha kwa viongozi husika ili zipatiwe ufumbuzi wa haraka.


Diana na wajumbe wa kamati hiyo ya ushindi walifanya kampeni sokoni hapo kwa kuwatembelea akina mama lishe,  wauza mazao mbalimbali, wauza kuku, wauza mbogamboga na matunda, bucha, waendesha bodaboda, Bajaji, washonaji nguo na wauzaji wa bidhaa za aina mbalimbali.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages