Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Elisha Elia unatarajiwa kuzikwa October 27, 2020 siku ya Jumanne mkoani Mbeya, Baba mzazi wa marehemu Elisha, Mzee Elia Mwakagali amesema.
“Msiba ulitokea jana saa 10 jioni Hospitali ya Taifa Muhimbili na leo tumekusanyika hapa nyumbani ndugu na jamaa tukijipanga kwa ajili ya safari ya kuelekea Mbeya alipotokea marehemu” Mzee Elia
“Ratiba ya leo mwili utawasili nyumbani mida ya saa 5 mpaka saa 6 na tutaelekea Kanisa la Kilutheri Segerea ambapo itafanyika ibada ya kuaga mwili na kutoa heshima za mwisho na ikifia saa 8 kamili tutaanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya na marehemu atazikwa Jumanne mchana,” Mzee Elia
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇