Mgombea wa Urais Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa dhamira yake ya kuwatumikia Wazanzibari iko imara tofauti na wakati mwingine huku akieleza kuwa kampeni za Urais zimemuwezesha kujua uzito wa dhamana ya nafasi hiyo anayoiomba.
Akizungumza na katika mkutano wa kufunga kampeni zake katika uwanja wa Demokrasia (Kibandamaiti) Dkt. Mwinyi ametaja idadi ya mikutano ya hadhara na isiyo ya hadhara aliyoifanya kuwa ni 75 visiwani humo.
“Ninaposimama kuomba kura ninasimama nikiwa na uelewa wa uhakika wa haja zenu, matamanio yenu na matumaini yenu halikadhalika kampeni hizi zimeniwezesha kutambua uzito wa dhamana wajibu unaoambatana na dhamana ya Urais ninaouomba” Dkt. Mwinyi
“Kuzunguka huku kumenipa fursa yakutafakari nakujipima tena na tena nimeridhika kuwa dhamira yangu yakuwatumikia wazanzibari iko imara sasa kuliko wakati mwingine wowote” Dkt. Mwinyi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇