Mgombea Udiwani Kata ya Gongo la mboto, Lucas Rutainura akiwa anafunga kampeni kwenye viwanja vya Kampala akiwaomba wananchi wampigie Kura Oktoba 28.
Mgombea huyo ameahidi kuwajengea soko wakazi wa Ulongoni, kuboresha miundombinu na kujenga kituo Cha afya.Aliwaomba wamchagueMgombea Urais wa chama hicho, Dk John Magufuli na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa ili waweze kuleta maendeleo kwa pamoja.
Kada wa CCM ambaye pia ni Mwanasheria, Nikson Tugara akijadili jambo na Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa wakati wa mkutano huo wa kampeni.
Baadhi ya viongozi wa Chadema Kata ya Gongo la Mboto wakirudisha kadi na kakabidhiwa kadi za CCM walipoamua kuhama na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇