Mgombea Ubunge jimbo la Kigoma mjini kwa tiketi ya CCM, Kilumbe Ng'enda akimjulia hali kijana Joseph Boniphace leo katika Hospitali ya Maweni mjini Kigoma. Kijana huyo alipata ajali ya gari jana akiwa katika msafara wa Mgombea Ubunge jimbo la Kigoma mjini Zitto Kabwe.
Kigoma mjini, Kigoma
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kigoma mjini, Kilumbe Ng'enda, leo asubuhi alimtembealea na kumjulia Kijana Joseph Boniface aliyepata ajali jana Oktoba16, 2020 katika Msafara wa Mgombea Ubunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Zitto Kabwe.
Kijana Joseph Boniface anaishi Kata ya Mwanga Kaskazini Mtaa wa Kisangani Jimbo la Kigoma Mjini, katika ajali hiyo amevunjika Mguu wa kushoto na amelazwa katika Hospital ya Maweni akipatiwa matibabu.
"Hali ya Joseph haikuwa nzuri alikuwa apelekwe katika chumba cha upasuaji kwa matibabu ya awali, Wakati wakiwa wanajiandaa kwa matibabu zaidi", amesema Kilumbe Ng'enda nakuongeza;
"Kwa bahati mbaya tangu alipopata ajali hiyo jana sio mgombea wala kiongozi yeyote wa ACT aliyepata nafasi ya kwenda kumuona.
Kwa kuwa anahitaji msaada wa kimatibabu, nimempatia msaada kidogo lakini bado Joseph anahitaji msaada zaidi ili aweze kusafirishwa kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Bugando".
"Kwa kuwa jambo hili la ajali ni la kibinadamu nitawaomba msaada marafiki zangu ili tushirikiane kumsaidia kijana huyu Joseph apate matibabu zaidi", amesema Kilumbe Ng'enda.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇