CCM Blog, Dar es Salaam
Hafla ya Mahafali na siku ya Wazazi (Atlas Day) ya Atlas Schools iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sasa itafanyika leo, Jumapili, Agosti 18, mwaka huu, mahafali yakihusisha wahitimu wa Madarasa ya saba ya Ubungo na Madale na Shule ya awali ya Atlas Schools iliyopo Ubungo, huku hafla hiyo ikitarajiwa kuhudhuriwa na waalikwa zaidi ya 15,000.
Awali hafla hiyo ilikuwa ifanyike wiki iliyopita Agosti 14, 2020 lakini Uongozi wa Atlas Schools ukaiahirisha kwa sababu ya kuheshimu ziara ya Rais Dk. John Magufuli ambayo aliihitimisha katika Mkutano wake uliofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe wiyala ya Kinondoni ambamo Atlas Schools pia ipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Atlas Sylivanus Rugambwa amesema, katika hafla hiyo iliyopangwa kuwa ya kipekee mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo badala ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambaye ametingwa na majukumu mwengine, na kwamba mgeni huyo rasmi atashiriki shughuli mbalimbali zitakazoambatana na hafla hiyo ikiwemo kuzindua daraja la Wananchi lililojengwa na Taasisi ya Atlas, kutoa medali kwa Washindi wa 'Atlas half Marathon' 2020 na kugawa vyeti na tuzo mbalimbali.
"Shule zetu zimejiandaa kiasi cha kutosha kuhudumia watu wote watakaohudhuria ikiwa ni wazazi, walezi, ndugu jamaa na marafiki utakaokuwa umeambatana nao kuja kushuhudia siku hii kubwa muhimu itakayopambwa na shughuli mbalimbali kwa watoto weto.
Amesema katika hafla hiyo Wanafunzi wote 810 watavaa nguo zao maalum tofautitofauti ambazo kimsingi zitakuwa mapambo ya siku na kwa upande wa waalikwa wanaume itapendeza zaidi kama watavaa suti nyeusi na tai nyekundu na kwa wanawake vazi lolote la heshima, wanafunzi wa kutwa wasioshiriki michezo watavaa nguo nadhifu za nyumbani na wanaoshiriki michezo mbalimbali na wabafunzi wa bweni watavaa sare zao za shule," amesema Rugambwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇