Kura hizo zimeombwa kwa makundi haya maalum wakiwemo *wajasiriamali, mamalishe,wauzaji wa mboga mboga ,bodaboda, wamiliki wa maduka, bucha na wapiga debe wa stendi ya Chang'ombe*
Kiongozi wa ziara hiyo ambaye ni mwenyekiti wa UWT wilaya ndugu *Winifrida Kaliyo* amewaasa vijana kutokuwa chanzo Cha kuleta vurugu kwa kutumiwa na wanasiasa hasa tunapoelekea kipindi hiki cha kupiga kura kwani amani ni tunu ya taifa hili.
Kwa upande wake katibu wa UWT wilaya *ndugu Diana Madukwa amewapongeza wananchi wa soko la Chang'ombe kwa mwitiko chanya kukubali kumpigia kura nyingi za ndiyo ndugu Magufuli ambapo wamesema wataishangaza dunia kuliko wakati wowote na historia itaandikwa kwani Magufuli atapata ushindi wa kimbunga.
Katika zoezi hilo picha za mgombea Urais wa CCM zimegombewa na makundi hayo pamoja na wateja wao huku wakiapa kupiga kura zote kwa wagombea wa CCM.
UWT inawashukuru viongozi wa soko hilo kwa ushirikiano wao mzuri.
Imetolewa na:
Diana Joseph Madukwa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇