WOTE tutakubaliana kwamba Tanzania ilishapoteza heshima linapokuja suala la usafiri wa anga. Baada ya kubaki na ndege moja tu mbovu ambayo hata hivyo haikuwa inafanya safari za maana, tuligeuza viwanja vyetu vya ndege kuwa maeneo ya kunufaisha mataifa mengine ya nje, hatukuwa na ndege.
Kuwa na shirika la ndege la Taifa ni zaidi ya kuwa na shirika la usafiri, linakwenda mbali ya hapo, ni utambulisho wa taifa, ni fahari ya wananchi na taifa lao, ni kichocheo kikubwa cha utalii, hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo ina vivutio vingi vya utalii.
Ndiyo maana suala la Tanzania kukosa ndege, ilikuwa ni agenda muhimu ya vyama vya upinzani katika chaguzi za nyuma, walifanya hivyo kwa kujua umuhimu wa taifa kuwa na shirika la ndege kwa ajili ya heshima na kielelezo cha uwezo wa kujitegemea kwa taifa husika.
Rais John Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015 miongoni mwa vipaumbele vyake ilikuwa ni kuirejeshea heshima Tanzania, mojawapo wa hatua hizo ni pamoja na kufufua shirika la ndege la Tanzania, ATCL.
Leo Tanzania tunajivunia kuwa ndege 11 zilizopatikana ndani ya kipindi cha miaka mitano, na umuhimu mwingine wa Tanzania kuwa ndege za umejionyesha wakati wa janga la korona. Pale ambapo dunia yote ilikuwa imejifungia, Tanzania ilituma ndege za shirika lake kuwachukua raia wake waliokuwa wamekwama India na kuwarejesha nyumbani.
Tanzania sasa imeuganishwa na safari za ndege, wananchi wanaweza kusafiri na kuwasiliana kwa haraka na hivyo kurahisisha huduma, badaala ya mtalaamu anayetakiwa Mpanda kwa mfano, kutumia siku nzima akisafiri kutoka Dra es Salaam, sasa atatumia saa chini ya mbili kufika na kutoa huduma inayotakiwa na kurudi.
Lakini kwa kuwa siasa zetu zimejaa wachumia tumbo, hao hao waliokuwa wanadai ni aibu Tanzania kutokuwa na ndege, baada ya kununuliwa na kufanya kazi kwa ufanisi, sasa wanazusha mambo mengi ya hovyo, ikiwemo shirika kutokaguliwi hesabu zake na kwamba linaendeshwa kwa hasara.
ATCL inadhihirisha unafiki wao, ndiyo maana hata wakati ndege zetu zinakamtwa badala ya kuungana pamoja kama Watanzania kutetea mali za taifa letu, wao walishangilia, na kwa unafiki wakawa wanaomba bila soni ndege zetu ziendelee kushikiliwa, kisa serikali ifedheheke ili wao wapate manufaa ya kisiasa.
Sasa baada ya shirika letu la ndege kujikwamua kutoka kwenye shimo la kufilisika na kusimama kama kampuni nyingine yoyote inayoweza kufanya biashara kwa ushindani, wameanza kuzua ushushi hatari. Eti wanasema hesabu za shirika hazikaguliwi, tena wanaongeza kwamba shrike linajiendesha kwa hasara kubwa na ni mzigo kwa walipo kodi wa Tanzania.
Sitaki kuamini kwamba wanaposema haya hawaujui ukweli ambao nitaueleza hapo baadae, kinachofabyika ni unafiki na udalali wa hoja za matifa makubwa ili kuivuruga Tanzania na msimamo wa Rais Magufuli wa kuiongoza Tanzania kuwa taifa linalojitegemea kikamilifu.
Wakati serikali imeanza juhudi za ufufuaji wa kampuni ya ATCL Oktoba, 2016 ilikuwa na miaka minane ambayo mahesabu yake yalikuwa hayajakaguliwa, kwa sababu ni kama haikuwepo.
Kazi ya kwanza ya Menejimenti mpya chini ya Mhandisi Ladislaus ilikuwa kuhakikisha hayo mahesabu yanakaguliwa, hata kama yamekaa miaka minane bila kukaguliwa.
Mahesabu yalivyokaguliwa wakaguzi walishindwa hata kutoa opinion (maoni), yalikuwa mahesabu ambayo hayawezi kuelezeka, yalikuwa yameshindikana kiasi cha wakaguzi kutoweza kutoa opinion. Kwa miaka hiyo minane ATCL ilikuwa inatengeza hasara ya shilingi bilioni 20 kila mwaka, ikiwa na madeni inayodaiwa yanayofikia shilingi bilioni 180.
Hesabu zilizofuatia zilikuwa za Juni 2017 hizo ndiyo zilikuwa za menejimenti mpya ambazo zilikuwa za kutoka Julai 2016 hadi Juni 2017, hapa uzingatie kwamba mpango wa kuifufua ATCL ulianza Oktoba 2016, lakini hesabu zilizokaguliwa ni kuanzia Julai 2016, kwa hiyo ule uozo wa Julai mpaka Oktba 2016 nao ukaingia kwenye hesabu za mwaka huo, baada ya kugakuliwa hasara ikapungua kutoka shilingi bilioni 20 mpaka bilioni 16.
Hapa lile deni la bilioni 180 liko pale pale, kwa tafsiri nyepesi ni kwamba linaingia kwenye vitabu vya hesabu na likiingia kwenye vitabu, kimahesabu riba ya deni inawekwa kwenye gharama za uendeshaji na ikiwekwa huko inakuwa matumizi hii inashusha faida yako, na hii riba kila mwaka inakuwa kama shilingi bilioni 9 kwa mujjibu wa assumption za wakaguzi.
Ukaguzi wa hesabu uliofuata ziliizishia Juni 2018 ATCL ikatoka kwenye hasara ya bilioni 16 mpaka bilioni 10, mwaka huo mapato yalipanda kutoka shilingi bilioni 23 hadi bilioni 54, lakini athari za ile riba ya karibu bilioni tisa inaendelea, kwa vyovyote unavyofanya kuna matumizi ambayo hayahusiani na wewe ukichukua hii shilingi bilioni 10 ukaitoa hii bilioni 9 ya deni la zamani ni kama hakuna hasara.
Kwa hesabu ambazo hazijakaguliwa za mpaka Juni 2019 hasara imeshuka kutoka bilioni 10 mwaka uliotangulia mpaka shilingi bilioni 4, lakini bilioni 9 ile iko pale pale na huenda inaongezeka maana ni cumulative.
Ukiangalia performance ni nzuri kwa uthibitisho wa hesabu zilizokaguliwa na anayekagua ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambaye ana kasimu jukumu hilo kwa kampuni inayoheshimika sana ya Pricewaterhouse Cooper (PwC).
Kwenye hesabu zilizoishia Juni 2018 ATCL ilipata hati safi kutoka kwenye mahesabu ambayo hawakuweza hata kupata opinion, ndani ya miaka mwili. Menejimenti ya ATCL imefanikiwa hivi kwa kuongeza mapato na kupunguza matumizi lakini bado inashikiliwa na yale madeni.
Kama serikali ikiweza kuyaondoa madeni haya, ni wazi kuwa shirika hili litafanya vizuri zaidi
Yakiondolewa haya na hiyo riba ya bilioni tisa ambayo sasa hivi inaeelzwa kukaribia bilioni 13 ATCL watakuwa vizuri, kwa sababu ukiangalia hesabu zilizoishia Juni 2018 waliyopata hati safi riba peke yake ilikuwa shilingi bilioni 11 halafu wakapata hasara ya shilingi bilioni 10.
Ukiangalia utendaji wa sasa ukiwianisha na huo mzigo wa madeni hakuna shaka kwamba wanafanya vizuri, lakini yale madeni kwa sababu yako kwenye vitabu vya ATCL mkaguzi hawezi akayaacha.
Ukiangalia mpango wa biashara wa ATC waliojipangia ni kwamba itakapofika mwisho wa mpango shirika wa miaka mitano, Juni 2022 wawe wame break even.
Kwa shiriki lilikokuwa likitengeneza hsara ya shilingi bilioni 20 kwa mwaka, kufuta hasara hiyo mpaka sasa shirika linaweza kujiendesha ni hatua kubwa sana, ukondoz na mzigo mkubwa wa madeni uliopo, bila shaka wajuvi wa mahesabu watabaini kwamba katika kipindi cha miaka chini ya mitano ATCL, wamefanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano.
Na yote haya bila woga lazima tukiri ni mafanikio ya uongozi shupavu wa Rais Magufuli, ambaye kwa dhamira ya dhati kabisa alijua moja ya hatua muhimu za kuijenga Tanzania inayojitegemea ni pamoja na kufufua kampuni za kimkakati kama ATCL.
Ndugu Tundu Lissu, kuzua uongo kuhusu kutokaguliwa kwa hesabu za ATCL au kwamba shirika linafanya kazi ya hovyo na ya hasara, siyo tu kwamba ni uzushi, lakini kwa mtu kama yeye anayewainia nafasi kubwa ya uongozi katika nchi hii, anachokifanya ni usaliti mbaya na hatari kwa mama Tanzania.
Mtu unataka kuwa rais kwa kudanganya watu unaotaka kuwaongoza ili iweje? sitaki kuamini kwamba ndugu yetu huyu hayajui mahesabu haya ya ATCL, wala siwezi sadiki kwamba hajui umuhimu wa taifa kuwa na shirika imara la ndege, anachofanya ni kutekeleza matakwa ya wanaotamani kutuhamisha kwenye jia sahihi ya maendeleo tuliyochagua.
Watanzania lazima tuanze kuwajua na kuwaepuka wanaotumia demokrasia kama kisingizio cha kutuondoa kwenye dhamira yetu ya kujenga uchumi imara unaotumia rasilimali za Tanzania kwa manufaa ya watanzania. Katka hili jemedari wetu Rais John Magufuli anastahili miaka mitano minngine tuendelee kusonga mbele kufikia malengo yetu.
*Magufuli5Tena*
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇