KADA wa CCM, Haji Manara (kulia), akimnadi mgombea udiwani Kata ya Kivukoni kwa tiketi ya CCM, Dotto Msawa, wakati wa mkutano wa ufunguzi wa kampeni katika Kata ya Kigamboni, Dar es Salaam.
NA MWANDISHI WETU
KADA wa CCM, Haji Manara, amewaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa jumla kujitokeza kwa wingi na kuipigia kura CCM ili ushindi uwe mnono tena wa kishindo.
Manara alitoa wito huo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Kivukoni, Dar es Salaa, juzi, kabla kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, Dotto Msawa.
Manara alisema uchaguzi wa mwaka huu ni mwepesi sana endapo wananchi watajitokeza kwa wingi kupigakura kwa kumchagua mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli pamoja na wabunge na madiwani.
"Tunataka kushinda kwa kishindo na kishindo chenyewe wapinzani wasahau uchaguzi miaka ijayo, maana yake aliyoyafanya Rais Dk. Magufuli ni mambo makubwa sana, mfano suala la corona alivyolishughulikia kwa kusema corona haiwezi kushinda nguvu ya Mungu na sasa kila mwananchi anaendelea na shughuli zake kiuchumi", alisema.
Alisema ni lazima tujitokeze kwa wingi kumpigia kura Rais Dk. Jihn Magufuli ili aweze kushinda pamoja na wabunge na madiwani wakasimamie miradi ya maendeleo kwa haraka.
Manara alisema Rais Dk. Magufuli, ameweza kuweka sawa uchumi wa nchi yetu, kwani endapo angeruhusu wananchi wasifanye shughuli zao wajifungie ndani kutokana na ugonjwa wa corona uchumi ungeshuka na wananchi wangekuwa na hali ngumu.
Kwa upande wa mgombea udiwani katika Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, akiwaomba wananchi kuipa kura CCM kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani ili aweze kutekelza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo.
Dotto alisema apewe kura ili akamalizie miradi iliyobaki ikiwemo ujenzi wa Shule ya Makonda ambayo aliijenga wakati akiwa diwani kwa kipindi kilichopita.
"Tupeni kura ili tukamalizie miradi ya maendeleo kwa haraka, kwani mkiwapa upinzani hawataweza kumaliza miradi hiyo kwani hawajui wapi kwa kupata fedha", alisema.
Alisema kuna barabara ya kiwango cha lami inajengwa kutoka Mikadi kwenda Sheraton ina urefu wa kilometa 1.6 pamoja na mifereji maji, ili itekelezwe lazima kuichagua CCM inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli.
Dtto alisema tumefanikiwa kujenga vituo vya afya katika kata hiyo na sasa huduma za mama na watoto zinatolewa kwa kiwango cha juu, yote hayo ni kutokana na utekelezaji wa Ilana ya CCM.
"Ndugu zangu wananchi wa Kigamboni naomba tuchague maendeleo, msifanye mchezo katika kuchagua watu, maendeleo ya Kigamboni mnatakiwa kuchagua watu thabiti na wenye upeo wa kuwangalia", alisema.
MSANII wa muziki Bongo fleva, Mbwana Kilungi 'Mbosso' akitoa burudani wakati mkutano wa kampeni katika Kata ya Kigamboni
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇