Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesisitiza ujio wa kipigo kikubwa kwa vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 28 mwaka huu.
Ameyasema hayo tarehe 05 Oktoba, 2020 akizungumza na Wazee Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.
"Jambo la msingi limetusaidia ni kuwa na wagombea ambao wanaweza kuanza na kufika mwisho wa kampeni ukilinganisha na vyama vingine, nimesikia kuna vyama vimeishiwa pumzi, wanaanza sasa kupanga hapa diwani awe wa chama kipi, maana wengine wapo chali, na wamefika mpaka ngazi ya Urais, wanawapumzisha wagombea fulani, ili waone upepo."
Akisisitiza uwezo wa CCM kushinda ameeleza,
"Hata wakihamisha pumzi kwa mmoja, kipigo kipo pale pale."
Katibu Mkuu akizungumza na wazee hao, licha ya CCM kuwa na uhakika wa ushindi mkubwa, amehoji utaratibu unaotumiwa na baadhi ya vyama vya upinzani kuunganisha nguvu baada ya wagombea wa vyama hivyo kuanzia ngazi za Udiwani, Ubunge na hata Urais kuanza kukata pumzi na kutoweza tena kuendelea na shughuli za kampeni.
Ameeleza kuwa, utaratibu unaotumika haujawahi kufanyika, na ni utaratibu unaodhihirisha wazi vyama hivyo kutokujiandaa na shughuli za kampeni, lakini kinachosikitisha ni vyama hivyo kuanza kujiandaa kulalamikia matokeo ya baada ya Uchaguzi tarehe 28 Oktoba, 2020 CCM itakapopigiwa kura za kutosha na kushinda kwa kishindo.
Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇