LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 22, 2020

WANANCHI WATAKIWA KUICHAGUA CCM WAZIDI KUPATA MAENDELEO


Na Scolastica Msewa, Mkuranga.

Wananchi wa Kata ya mwarusembe wilayani mkuranga mkoani pwani wameahidiwa kujengewa kituo cha afya ndani ya miaka mitano ijayo. 


Ahadi hiyo imetolewa na mgombea ubunge Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega wakati alipokuwa akiomba kura mbele ya wananchi hao na kusema zahanati inayojengwa kwenye Kata hiyo imekamilika na itafunguliwa mwezi December mwaka huu baada ya uchaguzi. 

Ulega amesema miaka mitano ijayo wamejipanga kwenda kutekeleza shughuli za maendeleo na moja ya mikakati waliyonayo ni kuifanya zahanati ya mwarusembe kuwa kituo cha afya na gari ya kubebea wagonjwa italetwa.

Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi ameongeza kuwa kikubwa cha kufanya kwa sasa ni kujenga nyumba ya mganga na  wodi ya kinamama ili kuwaondolea changamoto ya umbali kinamama wanapotaka kujifungua .

Aidha mgombea huyo amewatoa hofu wananchi hao kuhusiana na barabara yao ya  bigwa -kiziko kuwa inaenda kukarabatiwa km 6 kwa kuweka kifusi na tuta kwenye sehemu korofi kwasababu imeingia kwenye bajeti ya serikali. 

"Katika miaka mitano hii tunaenda kukamilisha zahanati ya bigwa, muda mfupi ujayo umeme utafika kitonga nimeshazungumza na naibu waziri wa nishati Subira Mgalu na ndugu wa kinene tunajenga shule pale Ili watoto wetu wapate kusoma pale!". Amesema Ulega 

Akizungumzia aliyoyafanya miaka mitano iliyopita mgombea huyo amesema ukiacha ujenzi wa zahanati na madarasa ametoa mashine mbili za kufyatua tofali vibao mia na lory nne za mchanga lengo kuwainua vijana  kiuchumi.

Sanjari na hayo ulega amesema katika miaka mitano hii aenaenda kukamilisha zahanati ya bigwa na muda mfupi ujayo umeme utafika kitonga na vijiji vingine vilivyobakia. 

Akizungimzia michezo wakati wa kampeni ulega amesema, ulega Cup itaendelea na vijana wote kila kijiji watapata jenzi na mpira,na vikundi vya kimama vitapewa kipaumbele katika suala zima la mikopo 

Aikiendelea na kampeni katika kata ya kiparang'anda ameahidi kutoa mil 1.5 kwajili ya ujenzi wa sehemu ya biashara ya wazee wa matunda .

Hata hivyo bararabara ya Kibanda baridi msolokelo ipo kwenye orodha rasmi ya serikali pale chini na tutaweka karavati mbez - msokelo na kusema kuwa ataunga mkono zahanati zote zilozoazishwa na madarasa yatajengwa.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages