LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 11, 2020

WAGOMBEA 16 WA URAIS ZANZIBAR WAPITISHWA NA ZEC, MAALIM SEIF AKWAA KISIKI

       Maalim  SeifShari Hamadi

Mgombea Urais wa Zanzibar Zanzibar kwa tiketi ya ACT- Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, amekwaa kisiki na hivyo kushindwa kuanza kufanya kampeni baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kushindwa kumpitisha kutokana na kuwekewa pingamizi.


Maalim Seif atakuwa huru na kupitishwa na ZEC atakapofanikiwa kudadavua na  kushinda pingamizi aliyowekewa kwa kujibu hoja zinazohusiana na pingamizi hiyo.


Maalim Seif amekwama huku ZEC ikiwa tayari imewapitisha wagombea 16 kati ya 17 waliomba kuteuliwa nafasi hiyo ya Urais na sasa wapo huru kuanza kufanya kampeni.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages