LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 11, 2020

MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA ADAIWA KUMILIKI BUNDUKI KINYUME CHA SHERIA

Singida

Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Mjini kupitia CHADEMA Rehema Mkoha (Pichani), amekamatwa na Polisi akiwa na watu wengine kumi kwa tuhuma za kumiliki silaha za moto kinyume cha sheria.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Sweetbert Njewike akizungumza kwa njia ya simu, alikiri kukamatwa kwa mgombea huyo na watu wengine kumi na kisha kuachiwa baada ya kuhojiwa ambapo watatakiwa kuripoti tena polisi leo Ijumaa, septemba 11, 2020.


Kamanda Njewike alisema kabla ya kuwakamata Polisi walifanya upekuzi ndani ya nyumba ya mgombea huyo baada ya kupata taarifa kuwa anamiliki silaha za moto.


"Tulipomkamata mgombea huyo na vijana wengine wanaoishi ndani ya nyumba hiyo tuliwaachia kwa dhamana na tunaendelea na uchunguzi tumewaambia waje leo tuwahoji," alisema Kamanda Njewike.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages