************************************
Viongozi Wa Dini Wa Kamati ya Amani wamelaani vikali vitendo vya baadhi ya Viongozi Wa Dini kutumia Madhabahu na Nyumba za ibada kufanya kampeni za kuwanadi viongozi Wa Dini jambo ambalo ni kinyume na maadili.
Akizungumza na waandishi Wa habari leo, Mwenyekiti Wa kamati hiyo ambae pia ni Sheikh Wa Mkoa Wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum amesema kama vitendo hivyo vitafumbiwa macho vinaweza kuhatarisha hali ya amani na kuwagawanya waumini wanaokwenda kusali.
Aidha amesema Kama kiongozi Wa dini anaona mgombea fulani anamfaa ni vyema akaenda kwenye majukwaa ya siasa ili kumnadi lakini sio kutumia nyumba za ibada kunadi wanasiasa.
Katika mkutano huo pia umehudhuriwa na Wajumbe Wa kamati ya amani ikiwemo Maaskofu, manabii, wachungaji, Maimamu na Mashaikh ambapo wote kwa pamoja wamaonyesha Kutokufurahishwa na vitendo hovyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇