LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2020

PRINCE DUBE AING’ARISHA AZAM FC UGENINI YAICHAPA 1-0 PRISONS NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU


 Na Mwandishi Wetu, SUMBAWANGA

TIMU ya Azam FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, wahamiaji Tanzania Prisons jioni ya leo Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji mpya kutoka Zimbabwe, Prince Mpumeled Dube dakika ya 90 akimalizia kwa kichwa kona iliyochongwa na winga aliyetokea benchi kipindi cha pili, Idd Suleiman ‘Nado’ kutoka upande wa kushoto.

Na kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 12 baada ya mechi nne ikirejea kileleni, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake nne baada ya mechi pia.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, mabao ya Marcel Kaheza dakika ya 11 na 61 na Tariq Seif dakika ya 33 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages