LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 14, 2020

UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA KAWE, GWAJIMA ASEMA HATAFAUTI UBUNGE KUGANGA NJAA, AAHIDI NEEMA TELE JIMBONI AKISHACHAGULIWA

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam, Askofu Dk. Josephat Gwajima, akijinadi na kuomba kura zake, Madiwani na za Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Rais Dk. John Magufuli, wakati wa uzinduzi wa Kampeni za CCM Uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Bunju A, jimboni humo jana. 

Akijinadi Gwajima alisema hakujitokeza kugombea Ubunge ili 'agange njaa', bali anauhitaji Ubunge wa Jimbo hilo kwa kuwa amesukumwa na shauku ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Amesema, pia haombi Ubunge kwa ajili ya kwenda Bungeni kama Askofu ili kutangaza neno la Mungu, bali anaomba kwenda Bungeni kuitumikia jamii kama mwananchi anayeguswa na kuwaletea wananchi maendeleo.

"Mimi na huyu mwenzangu Abbas Tariba anayegombea Ubunge pale Kinondono, hatutafuti Ubunge ili tugange njaa kama wengi (Wapinzania) walivyo, sisi tunakuja kuwatumikia wananchi katika kuwainua kimaendeleo na wakati mwingine tutatumia gharama zetu", alisema Gwajima huku wananchi mkutanoni wakilipuka kumshangilia.

"Tazameni mimi nimeshafanya mengi kwa gharama zangu kama kuchimba visima vya maji na kuyapeleka hadi kwenye Misikiti ya wenzetu Waislam na wananchi wengi tu...sasa kama nilifanya hivi tena wakati sijaota hata kuomba ubunge, mkinichagua nikawa Mbgunge wenu itakuwaje?, " Gwajima alisema na kuhoji halaiki.

Gwajima aliendelea kuahidi neema tele kwa wananchi wa Kawe akisema atasaka na kufungua fursa za ajira hasa kwa vijana na kina mama.

Wananchi wakimshangilia Gwajima wakati akiwahutubia katika mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Bunju A, jana
"Nimetembea maeneo mengi katika jimbo la Kawe, barabara nyingi za ndani ni mbaya, hazipitiki vizuri, mkishanichagua nikawa Mbunge nitanunua greda na lori kwa ajili ya kutengeneza barabara hizi, wakati wa utengenezaji wa barabara hizi vijana na kina mama watapata ajira", anasema Gwajina.
Wananchi wakimshangilia Gwajima  baada ya kutamka ahadi hizo
"Hawa wanapozungumza kuhusu mimi wanadhani wanamsema 'kilaza', mimi siyo kilaza nimesoma kwa kiwango cha juu kabisa tena ni katika mambo yanayohusu uchumi, maendeleo na ustawi wa jamii. Nilipokwenda Japan niliahidiwa kupewa meli kumi za uvuvi, hizi nitazileta hapa Kawe maana tupo karibu na Bahari, vijana watafundishwa namna ya kuzitumia kufanya uvuvi. Je hii siitakuwa fursa bora ya ajira na kuinua uchumi kwa vijana, kina baba na kina mama?" alisema Gwajima.
Baada ya kutamka maneno hayo wananchi wakalipuka tena kumshangilia.
Gwajima akiendelea kutoa 'madini' jukwaani.
Wananchi nao wakiendelea kumshangilia
Mwenyekiti wa Umoja wa Viajana wa CCM Heri James ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, akiunguruma jukwaani wakati akizindua rasmi Kampeni za CCM Jimbo la Kawe, jana. Akasema, " CCM haikumteua Gwajima kugombea katika Jimbo hili la Kawe kwa sababu ni Askofu, la hasha, tumemteua kwa sababu Chama kinamjua, ni mchapakazi, siyo mwonga, ni mweledi, mpenda manedeleo na kadhalika" 

Wananchi wakalipuka kumshangilia James baada ya maneno hayo

Gwajima akiwa amesimama na kupunga mkono baada ya Heri James 'kumfagilia' kwenye mkutano huo.
Wananchi nao wakawa wanasikiliza kwa makini hotuba ya James
"Gwajima ndiyo huyu hapa. mmemuonaaaa! mtampa kura yeye, madiwani na Rais Magufuliiiiiii?", akasema James, wananchi wakajibu " Tutawapaaaa", huku wakiinua mikono kuthibitisha
Umati wa wananchi ukiwa umesheheni kwenye mkutano huo
Gwajima akisubiri kwa unyenyekevu kupokea Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, kabla ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM Heri James ambaye pia ni Mjumbe wa kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, wakati wa mkutano huo.
Kisha Heri James akamkabidhi Gwajima Ilani hiyo
Gwajima akiionyesha Ilani ya CCM baada ya kukabidhiwa
"Naam Ilani ndiyo hii, kila ninachofikiri kukifanya kwa ajili ya Kawe tayari kimeandikwa humu", Gwajima akionyesha ilani hiyo na kuonekama kama anasema hivyo.
"Sasa sikiliza Chama kimeshakupatia Ilani, hakina shaka na wewe, nina imani utachaguliwa tena kwa kishindo, nenda ukaitekeleze", inaonekana ndivyo Heri James alivyokuwa akimwambia Gwajima.

MWANZO WA MKUTANO👇👇
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni Sure Mwasanguti akitangaza ratiba ya mwenendo wa Mkutano huu. Mbele ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi akiongoka baada ya kuzungumza jukwaani.
Katibu Mkuu wa UWT Queen Mlozi alipokuwa akizungumza jukwaani
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kinondoni Abbas Tarimba akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa kwenye mkutano hup
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Sure akiandika baadhi ya mambo wakati akisimamia mkutano huo mambo yaende kama yalivyopangwa.
Sheikh akiomba dua mkutano upate baraka za Allah
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Mama Hangaya akiomba sala kwa niaba ya wakristu Mungu aujaalie mkutano kwenda salama salmini.
Katibu wa CCM na Mlinzi wa Usalama Jukwaani wakipokea sala hiyo
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni Komredi Sure akimkaribisha mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kufungua mkutano huo
"CCM Oyeeee", Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Komredi Maruma akisema wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam kufungua Mkutano huo
"Wana Kawe nawasihi sana msifanye makosa kama mliyofanya wakati uleeee, safari hii kura zote kwa Ndugu magufuli, Gwajima na Madiwani wooote", Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akasema hayo wakati akifungua mkutano huo
Aliyekuwa mtia nia ya Ubunge jimbo la Kawe Ndugu Angela Kizigha akiteta jambo la mweneyekiti wa UVCCM Heri James jukwaani katika mkuatno huo. Kulia ni Dk. Gwajima na kushoto ni Komredi Maruma
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati ule mgeni rasmi Heri James alipokuwa akienda kuhutubia na kumnadi mgombea ubunge jimbo la Kawe kwenye mkutano huo.
Komredi Sure na Mama Kizigha wakijadiliana jambo. Kizigha ni miongoni mwa waliokuwa watia nia ya Ubunge jimbo la Kawe, ambaye alionyesha kuchakarika sana kwenye mkutano huo
Wageni mashuhuri wakiwa meza kuu kwenye Mkutano huo
"Hapa mambo yameenda vizuri sana", inaelekea ndivyo Kheri James alivyokuwa akimwambia Angela Kizigha wakati wakiteta. Kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Kawe Askofu Dk. Gwajima akiwasikiliza kwa makini.
Heri James akiwasalimia baadhi ya madiwani wanaogombea kata mbalimbali katika jimbo la Kawe baada ya kuwapandisha jukwaani
Wagombea Udiwani kumi katika kata mbalimbali za Jimbo la Kawe wakiwa jukwaani wakati wakitambulishwa na kuombewa kura  kwa wananchi na Mwenyekiti wa UVCCM heri James mwishoni mwa mkutano hu. (Maelezo na Picha zote na Bashir Nkoromo, Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages