Mambo yameiva jijini Dodoma, baada ya The Capital Park kioo cha maraha kuzinduliwa Iringa Road mkabala na Nala ambapo kuna kila aina ya starehe. Mahali hapo unaweza kupata huduma za kila aina zitakazokufanya uondoe uchofu baada ya majukumu yako ya kila siku.
Pia eneo hilo linaweza kukuondolea Stress kwa kuangalia matukio mbalimbali ikiwemo michezo kupitia Screen 11 zilizosambazwa kila kona ya eneo hilo. Pia kuna Counter za kisasa zilizosheheni vinywaji vya kila aina.
Vilevile pana jiko la kisasa lenye vyakula vya kila aina pamoja na nyama choma za mbuzi, kuku, ng'ombe na michemsho. The Capital Park ina eneo kubwa la kuegesha magari na vyombo vingine vya moto vyote huku vikilindwa na vijana maalumu ili kumhakikishia usalama mywaji.
Vile vile kuna wahudumu wanaopokea wateja kwa bashasha na kuwapatia huduma kwa haraka. Nje kuna huduma ya Taxi, Bajaji na Bodaboda waliovalia vijaketi vyenye jina la The Capital Park. HABARI,PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
Moja ya Counter za kisasa ikiwa imesheheni vinywaji vya kila aina. Counter hiyo ina Screen nne ambapo kila upande alipokaa mteja anaweza kuangalia tukio.
Wateja wakila bata
Ukiwa kwenye kiota hicho utaburudishwa na muziki poa unaoporomoshwa na Ma DJS Jab na Eddo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇