Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ,33 amekubali mkataba wa miaka mitano na kampuni ya soka ya City Group ulio na thamani wa £623m ambapo nyota huyo atahudumu misimu mitatu katika klabu ya Manchester City kabla ya kujiungana na ligi ya Marekani ya MLS akiichezea klabu ya New York City FC.
Paris St-Germain imeahidi kutoa pauni milioni 25 pamoja na pauni milioni 5 za ziada-kwa beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin, huku Bayern Munich na Juventus pia zikionesha nia ya Kumsajili mlinzi huyo wa Uhispania, 25. (Guardian)
Chelsea imesema thamani ya N'Golo Kante ni pauni milioni 80 huku Inter Milan ikionesha nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 29. (Express)
Hata hivo, mchezaji huyo aliyekuwa Leicester Kante hana mpango wa kuondoka Chelsea. (Goal)
Leicester imekubali kufikia makubaliano ya pauni milioni 22 kumsajili beki Mbeligiji Timothy Castagne, 24, kutoka Atalanta. (Telegraph)
Thomas Partey wa Atletico Madrid, 27, anataka sana kuhamia Arsenal lakini Gunners inahitajika kuachilia wengine kuhama kwanza kabla ya kutimiza kigezo cha kumsajili kiungo huyo wa kati raia wa Ghana anayesemekana kwamba thamani yake ni pauni milioni 44.5. (Goal)
Monaco inamnyatia kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucoure baada ya Everton kushindwa kuafikiana kwa dau linalohitajika kumsajili. (Evening Standard)
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 23 ambaye usajili wake uliweka historia. (Sun)
Newcastle inajaribu kufikia makubaliano ya Callum Wilson, 28, wa Bournemouth ambayo yatamuwezesha winga wa Scotland Matt Ritchie kujiunga na Cherries, lakini Aston Villa pia inamnyatia mshambuliaji huyo wa England. (Sky Sports)
PSG imewasiliana na winga wa Inter na Slovakia Milan Skriniar, 25, ambaye pia Tottenham inammezea mate. (Calciomercato - in Italian)
Crystal Palace imekataa ofa ya pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji wa Norway Alexander Sorloth, 24, kutoka RB Leipzig. (Mail)
Juventus inataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Uruguay Luis Suarez, 33, au wa Roma, Bosnia Edin Dzeko, 34. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Mlinda lango Kepa Arrizabalaga, 25, yuko tayari kusalia Chelsea na kuendelea kupigania nafasi yake, hata ikiwa klabu hiyo itafanikiwa kumsajili mlinda lango mpya. (Telegraph)
Al Nassr imetoa ofa ya euro milioni 20 kwa mchezaji wa Arsenal raia wa Ujerumani Mesut Ozil, 31, sawa na pauni milioni 18 katika mkataba wa kujiunga na klabu hiyo ya Saudi Arabian. (Fanatik - in Turkish)
Tottenham imemtangaza aliyekuwa mwenyekiti wa Swansea Trevor Birch kuwa mkurugenzi wao mpya wa masuala ya soka. (Evening Standard)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇