Baba yake Lionel Messi na wakala wake, Jorge, wamekutana na rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu, aliyesema kwamba klabu hiyo haitafanya mazungumzo ya kumuuza mshambuliaji huyo wa Argentina, 33. (Marca)
Mkutano wa kwanza tangu Messi kutoa ombi la kuondoka klabu hiyo ukiishia bila makubaliano huku Barcelona ikisema ofa ya miaka miwili kwa mchezaji huyo bado ipo. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kima cha malipo ili Messi aruhusiwe kuondoka Barcelona huenda kikawa kidogo pengine hata euro milioni 100. (Telegraph)
Manchester United imealikwa katika majadiliano na Bayern Munich kuhusu kiungo wa kati Thiago Alcantara, 29. (ESPN)
Kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman anataka klabu hiyo kufanya kila linaloweza kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 29. (ESPN)
Aston Villa inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Newcastle katika mbio zake za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na England Callum Wilson, 28. (Telegraph)
Paris St-Germain imepunguza fursa ya uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa, Matteo Guendouzi, 21, kutoka Arsenal. (Telegraph)
DC United imechukua hatua ya kumtafuta mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, na pia inamnyatia kiungo wa kati wa Everton kutoka Iceland, Gylfi Sigurdsson, 30. (The Athletic - subscription required)
Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Gonzalo Higuain amepata ofa kutoka Ufaransa, England, Uhispania na China, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo. (Tuttosport - in Italian)
Watford huenda ikafikiria kumruhusu mshambuliaji Troy Deeney, 32, kuhamia kwingine kwa mkopo na kumrejesha ikiwa watapandishwa daraja tena katika Ligi ya Primia. (Telegraph)
Mlinzi wa Uhispania Eric Garcia, 19, anasema ataondoka Manchester City mkataba wake utakapoisha mwisho wa msimu. (Sun)
West Brom imeimarisha juhudi zake za kumtafuta winga wa England wa anayekipiga katika kikosi cha umri wa chini ya miaka 21 Grady Diangana, 22, kwa kutoa ofa kwa West Ham, makubaliano ambayo huenda yakapandisha kima chake hadi pauni milioni 18 huku kukiwa na uwezekano wa kima hicho kuengezeka zaidi. (Guardian)
Washambuliaji wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles na Kieran Tierney, wote wakiwa na umri wa miaka 23, watasalia klabu hiyo baada ya kocha Mikel Arteta kusema wazi kwamba anataka wawe sehemu ya kikosi chake. (90mins)
Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 21, ameombwa kusalia katika klabu hiyo na chanzo ambacho si cha kawaida... WWE wrestler Triple H. (BT Sport)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇