NA NEEMA MBUJA, KIBAHA
Shirika
la umeme Tanzania TANESCO kupitia Idara ya masoko imeendelea na kampeni ya
kutoa Elimu kwa wamiliki wa viwanda,machimbo ya madini, na mashine za kusaga
kwa mkoa wa Pwani ili kuwapatia Elimu juu ya matumizi Bora ya umeme sanjari na
kukagua miundo mbinu ya umeme pamoja na mota zinazotumiwa kwenye kuendesha
mashine.
Miongoni
mwa Elimu wanayopatiwa Ni pamoja na namna ya kutumia vifaa ambavyo vinatumia
umeme kidogo, umuhimu wa kukagua mota zao Mara kwa Mara kwa ajili ya kuleta
ufanisi na Usalama wa miundo mbinu
Akizungumza na wamiliki wa viwanda kwenye Wilaya za Chalinze, Mlandizi, na Kibaha, mhandisi wa umeme kutoka idara ya AMR mita Hassan Kipende amesema kuwa kwa Sasa baadhi ya viwanda vinatambua umuhimu wa kufunga power factor ingawa baadhi bado hawajatambua
Kuhusu wachimbaji wadogo wa mawe eneo la Chalinze mhandisi Kipende ameshauri kuendelea kuwapatia Elimu ya umuhimu wa kutumia umeme kwani wengi wao bado wanatumia mafuta kuendesha mitambo ya kuchakata mawe Jambo ambalo Ni hasara kwao
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇