Pia katika uzinduzi huo, Mavunde ambaye wakati wa ubunge wake ameshajenga visima 11, akichaguliwa tena ameahidi kuchimba visima vingi zaidi kwa gharama zake. Pia amesema kuwa utaratibu upo tayari kulipwa fidia kwa wenye maeneo patakapojengwa Uwanja wa Ndege wa Msalato na barabara ya njia nne itakayojengwa kuzunguka Jiji la Dodoma.
Wafuasi wa CCM wakiwa na moja ya mabango katika uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini.
Antony Mavunde akijinadi yeye na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli pamoja na wagombea udiwani 41 wa Kata zilizomo katika Jimbo hilo. Wananchi wakimchagua ameahidi kuongeza ujenzi wa shule zingine katika jimbo hilo. Hivi sasa ameshajenga shule mbili nje ya mfumo wa serikali.
Jackline Mavunde akimuombea kura mumewe Antony Mavunde ambaye ni mgombea ubunge jimbo la Dodoma Mjini. Aliyebebwa ni mtoto wao Atala.
Mavunde akimtambulisha rafiki yake wa siku nyingi Steven Masele aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Babake Antony Mavunde, Peter Mavunde akitambulishwa wakati wa mkutano huo.
Mavunde akikabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kibakwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akionesha kwa wananchi kadi ya kupigia kura ambapo aliwataka wazitunze vizuri hadi siku ya Oktoba 28, 2020 waende wakampigie kura mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, Mgombea Ubunge wa CCM, Antony Mavunde na madiwani 41 wa chama hicho.
Mavunde akimshukuru Simbachawene kwa kumnadi.
Sheikh Kisusu akiongoza kuwaombea dua wagombea akiwemo Mavunde (kulia) , Dk. Magufuli na madiwani. Pia aliombea amani Uchaguzi Mkuu.
Kikundi cha Life Music kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo. Zaidi ya vikundi vya sanaa 40 vilituiza katika uzinduzi huo.
Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia CCM, Mariam Ditopile akielezea kwa wananchi mambo mbalimbali waliyoyafanya kwa ufanisi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli hivyo kuwaomba ifikapo Oktoba 28, 2020 kuwapigia kura.
Wafuasi wa CCM wakishangilia baada ya kufurahishwa na ahadi alizokuwa anazitoa mgombea ubunge wa Jimbo Dodoma Mjini, Mavunde ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa msaada wa kompyuta katika shule za msingi na sekondari zilizomo katika jimbo hilo.
Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia CCM, Fatma Toufiq akiwamwagia sifa wagombea wa CCM, Dk John Magufuli (Urais), Antony Mavunde (ubunge) pamoja na madiwani na kuwaomba wananchi siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 wawapigie kura nyingi za ndiyo.
Masele ambaye aligombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika kura za maoni lakini jina lake halikurudi. akiwanadi mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. Magufuli na Mgombea ubunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini.
Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Mavunde , Mgombea Ubunge Viti Maalumu, Mariam Ditopile (kushoto), pamoja na Simbachawene (wa pili kulia) wakisakata muziki wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Ni burudani kwa kwenda mbele
Mavunde akikumbatiana na aliyekuwa Mgombea Ubunge katika kinyang'anyiro cha kura za maoni, Mussa Luhamo ambaye alikuwa anazungumza kwa niaba ya waliokuwa wagombea na kushindwa. Alisema wamevunja kambi zao na kuamua kushirikiana kuwapigia kura wa CCM, akiwemo Mavunde, Dk. Magufuli na madiwani
Ni furaha kwa kwenda mbele |
Bendi ya Mbukweni ikitumbuiza kwa wimbo wa CCM wakati wa kampeni hizo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa CCM, Tija Maayoma akielezea kazi kubwa zilizofanywa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Magufuli na Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Mavunde, hivyo kuwaomba wananchi kuwapigia kura, Magufuli na Mavunde Oktoba 28, mwaka huu
Msanii Ben Paul akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇