LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 3, 2020

SPIKA JOB NDUGAI AZINDUA JENGO LA TAKUKURU WILAYA YA MANYONI

 


Spika wa Bunge, Job Ndugai (watatu kulia) akikata utepe wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida. Watatu kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja (wapili kulia) na Mbunge wa Manyoni Magharibi, Mhe. Yahaya Masare.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na viongozi wa wilaya, watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza na watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali (hawapo kwenye picha) kabla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Mkurugenzi wa uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja akizungumza na viongozi wa wilaya, watumishi wa TAKUKURU na wageni mbalimbali (hawapo kwenye picha) kabla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.Spika wa Bunge, Job Ndugai akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwa ajili ya kuzindua jengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa baada ya kuzindua jengo la Taasisi hiyo Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida. Wapili kushoto waliokaa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa  Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa (kushoto waliokaa) na Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Ndg. Sabina Seja (wapili kulia waliokaa)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages