LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 16, 2020

RAIS MAGUFULI ASISITIZA KUTOONGEZA HATA SIKU MOJA ATAKAPOMALIZA MUDA WAKE WA MIAKA 10


Rais Dk. John Magufuli akiwa kampeni zake kuomba rudhaa ya kuwaongoza Watanzania kwa miaka mingine mitano.

Bukoba, Kagera

Rais Dk. John Magufuli ambaye yupo katika Kampeni kuomba ridhaa kwa Watanzania kuliongoza Taifa kwa miaka mingine mitano, amesema hataongeza muda wa kuwa Rais tena atakapomaliza kipindi cha miaka yake kumi, badala yake atampisha mwingine ndani ya Chama Cha Mapinduzi andeleze atakapokuwa ameishia.


Dk. Magufuli ametamka hayo Septemba 15,2020, akiwa njiani kwenda mkoani Kagera kuendelea na mikutano yake ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu ulipangwa kufanyika Siku ya Jumatano, Oktoba 28 mwaka huu, kauli ambayo ameisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba akimaliza miaka yake mitano ijayo hataki kuongeza muda hivyo anaomba apewe miaka mitano mingine ili afikishe miaka kumi tu.


"Alikuwepo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alitutoa kwenye Ukoloni akatuongoza kisha akapumzika, akaja Mzee Hussein Mwinyi nae akaendelea na ruksa akafanya kazi yake kwa miaka kumi angeweza kuendelea lakini alisema imetosha, Akaja Mzee Mkapa akamaliza miaka yake kumi akapumzika, akaja Mzee Jakaya Kikwete akafanya kazi miaka 10 naye amepumzika, na mimi nimekuja nimefanya miaka yangu mitano, sasa naombeni tena niongezewe miaka mitano ile iliyobaki nikafanye maajabu kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii." alisema Dk. Magufuli na kuongeza. "Nataka kipindi hicho kikifika na mimi nipumzike kuangalia wenzangu wanavyofanya kazi".

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages