LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 13, 2020

NEC YATOA UAMUZI WA RUFAA 60 ZA WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI

 



Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha jana tarehe 10 Septemba 2020 imepitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa Wasimamizi mbalimbali wa Uchaguzi nchi nzima.

Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa Ubunge na Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.

Katika kikao hicho, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 60 kati ya hizo rufaa 2 ni za Wagombea Ubunge na 58 ni za Wagombea Udiwani. Matokeo ya rufaa za wagombea Ubunge ni kama ifuatavyo:
i. Imekubali rufaa moja na kumrejesha mgombea katika orodha ya

wagombea. Rufaa hiyo ni kutoka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi.
ii. Imekataa rufaa moja ya mgombea ambaye uteuzi wake

ulitenguliwa. Rufaa hiyo ni kutoka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi.

Aidha, Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 58 za Madiwani, kama ifuatavyo:
i. Imekubali rufaa 34 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya

wagombea Udiwani. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Kata za Kahororo (Bukoba), Ishozi (Nkenge),Chongoleani (Tanga Jiji), Kirare (Tanga Jiji), Mwamanga (Magu), NgĘ»haya (Magu), Riroda (Babati Vijini), Maswa Magharibi (Maswa), Kirumba (Ilemela), Bonga (Babati Vijini), Kamagambo (Karagwe), Namelock (Kiteto), Masewa (Bariadi), Bweranyange (Karagwe), Kituntu (Karagwe), Kamagambo (Karagwe), Msowero (Kilosa), Lubugu (Magu), Lingeta (Meatu), Ifakara (Kilombero), Kiloli (Sikonge), Mkoma (Rorya), Nyamhongolo (Ilemela), Sikonge (Sikonge), Tanganyika (Muheza), Uhenga (Wanging’ombe), Babati (Babati), Vwawa (Mbozi), Lukanga (Mkuranga), Langai (Simanjiro), Lutale (Magu), Majohe (Ilala), Namabengo (Namtumbo) na Viwanja Sitini (Kilombero). 

ii. Imekataa rufaa 23 za wagombea ambao hawakuteuliwa. Rufaa hizo

ni kutoka kwenye Kata za Ilemela (Ilemela), Kayenze (Mwanza Jiji),

Kiarare (Tanga Jiji), Mabawa (Tanga Jiji), Ilemela (Ilemela), Kadoto (Maswa Magharibi), Iyela (Mbeya Jiji), Kirua Vunjo Magharibi (Vunjo), Mji Mpya (Morogoro Mjini), Pugu (Ukonga), Tembela (Mbeya Mji), Vikumburu (Kisarawe), Mecco (Ilemela), Kibara (Mwibara), Kiloleli (Sikonge), Changarawe (Mafinga Mji), Igawilo (Mbeya Mjini), Msonga (Mkuranga), Uru Kaskazini (Moshi Vijini), Kivukoni (Ilala), Maanga (Mbeya Mjini), Nsalaga (Mbeya Mjini) na Jangwani (Ilala).

iii. Imekataa rufaa 1 ya kupinga walioteuliwa. Rufaa hiyo ni kutoka

kwenye Kata ya Arri (Babati Vijijini).

Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume kufikia 113 na za wagombea Udiwani 103. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages