LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 13, 2020

ARSENAL YAANZA VYEMA ENGLAND, YAICHAPA 3-0 FULHAM CRAVEN COTTAGE

 

ARSENAL imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Fulham waliorejea msimu huu, mabao ya Alexandre Lacazette dakika ya 18, mchezaji mpya Gabriel Magalhaes dakika ya 49 na Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 57 Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
Huo ni mwendelezo mzuri wa matokeo ya timu chini ya kocha Mikel Arteta msimu mpya, wakitoka kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 5-4 kufuatyia sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Liverpool Agosti 29 Uwanja wa Wembley Jijini London.

Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la tatu leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages