LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 4, 2020

MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA ITV AGNES ALMAS KUAGWA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM


Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV Agnes Almasi (Pichani) aliyefariki jana mchana wakati akijiandaa kwenda kazini utaagwa kesho kabla ya kusafirishwa kwenda Tanga kuzikwa.


Taarifa iliyosambazwa leo imesema, mwili wa marehe Agnes utaagwa katika Kanisa la St. Nicolas Anglikana lililopo jirani na kituo cha daladala karibu na Hospitali ya Amana, Ilala Jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwili utafikishwa kwenye Kanisa hilo kati ya saa 4 hadi saa 5 asubuhi ambako ibada itaambatana na kuagwa mwili hadi saa 8 mchana.

 

"Baada ya hapo itafuatia safari ya kusafirisha mwili kwenda Tanga kwa ajili mazishi yakayofanyika keshokutwa Septemba 6, 2020" Taarifa imesema na kuongeza kuwa taarifa za taratibu zaidi zitaendelea kutolewa.


Agnes alifariki dunia akipelekwa hospitali ya Amana, baada ya kujisikia vibaya wakati akijiandaa kwenda kazini akiwa nyumbani kwao Ilala. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages