LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 4, 2020

JK AWAASA WANACCM KUWA NA UMOJA NA MSHIKAMANO

 


Na Scolastica Msewa, Chalinze.

Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amewataka wanaCCM kuwa na umoja na mshikamano kwa ajili ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba 28 mwaka huu.


Amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Mgombea Mwenza wa chama cha Mapinduzi CCM Mama Samia Suluhu Hassani katika viwanja vya Chalinze wakati alipopewa nafasi ya kusamia wananchi kabla ya mgeni rasmi huyo kuhutubia.


Amesema wana CCM wajenge umoja na mshikamano kwani kila kitu kina utaratibu wake na mchakato wake ambapo hatua za uteuzi wa wagombea wa ubunge na udiwani ndani ya chama zimeshamalizika tayali mgombea ubunge na wagombea Udiwani wameshapatikana hivyo sasa wana CCM wanatakiwa kuwa na umoja kupiga kampeni CCM kipate ushindi.


“Sasa letu moja kumpigania mgombea wetu wa Urais, mgombea mwenza, mgombea ubunge na wagombea wetu wa udiwani ili wapate ushindi kwani Umoja ni ushindi ili CCM kidumu madarakani” alisema Rais mstaafu Dr. Jakaya Kikwete.


Alisema Kikwete “kuendeleza nongwa za michakato ya kura za maoni ni kujimaliza kisiasa ambayo itakuwa sawa na vita vya panzi ni furaha na neema ya kunguru”.


Aidha amewataka wana CCM kumpigania mgombea Urais wa CCM apate kura nyingi za kishindo zaidi ya asilimia 84 alizopata mheshimiwa Magufuli mwaka 2015 sasa ipate asilimia zaidi ya 90.


Mgombea ubunge wa jimbo la Chalinze anayetetea nafasi yake Riziwani Kikwete amemuomba Makamu wa Rais mama Samia kuangalia namna ya kuwaongezea ardhi wananchi wa vijiji vinavyozunguka katika msitu wa Zigua kwaajili ya shughuli za maendeleo.


“Kuna moja ya zahanati kwenye vijiji hivyo imechukuliwa na hifadhi hiyo ambapo hata mwananchi akiokota kuni msitu huo hupelekea kukamatwa jambo ambalo husababisha uhasaama kati ya wananchi na watumishi wa hifadhi hiyo” alisema Riziwani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages