Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Okash akifanya kampeni katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Soya. |
Mgombea Udiwani Kata ya Soya kupitia CCM, Mashaka Mashaka (kushoto), akinadiwa na Okash kwa wananchi wakati wa mkutano huo wa kampeni. |
MGOMBEA Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Okash amewaomba wananchi kumpigia kura za tsunami Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli Oktoba 28, mwaka huu, ili kumlipa wema kwa mambo makubwa aliyoifanyia Tanzania.
Okash alitoa ombi hilo kwa unyenyekevu huku akiwa amepiga magoti, alipofanya mikutano ya ndani na ya hadhara katika Kata ya Soya, wilayani Chemba, Dodoma.
"Msidanganyike kabisa na vyama vingine, kwani maendeleo yameletwa na CCM na yataendelea kutekelezwa na CCM. Tumlipe wema Dk. Magufuli aliyeifanyia mambo makubwa Tanzania kwa kumpigia kura za Tsunami Oktoba 28, 2020, kwani wema hulipwa kwa wema,"alisema Okash.
Akiwa katika kata hiyo, Okash alifanya vikao vya ndani kwa viongozi wa kata, vikao na wanawake na hatimaye kwenye mkutano hadhara ambapo alielezea mambo mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. Magufuli.
Alitumia fursa ya vikao hivyo kuwaombea kura pi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chemba, Mohammed Monni na Mgombea Udiwani wa Kata ya Soya, Mashaka Mashaka.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇