LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 21, 2020

MPEMBENWE AAHIDI KUSHUGHULIKIA UKAMILISHAJI UJENZI KITUO CHA AFYA CHA RUALUKE CCM KISHINDA TENA KIBITI

 

Mgombea Ubunge Jimbo la Kibiti Twaha Mpembenwe akiwa na wapigakura wake wakati akiwaomba kura katika kampeni zake.


Na Scolastica Msewa, Kibiti

Mgombea Ubunge wa Jimbo la kibiti mkoani Pwani Twaha Mpembenwe ameahidi kushughulikia kukamilika kwa kituo cha afya cha kata ya Rualuke ambacho kimeanza kujengwa tangu mwaka 2007 kwasasa kipo kwenye hatua ya ukamilishaji huduma zianze kutolewa iwapo CCM itapata dhamana ya kuongoza tena.


Akihutubia wananchi wa kijiji cha Rualuke tarafa ya Kikale Mpembenwe amesema kituo hicho cha afya ni muhimu kwa wananchi kwani hutembea kilo mita 32 kufuata huduma za afya hadi mji Kibiti huku tayali wananchi wamejitolea nguvu kazi ili kupata huduma za afya karibu tangu miaka 12 iliyopita.


Amesema wananchi waipe dhamana serikali ya CCM ili wakimalizie kituo hicho cha afya kwa kujenga na kuleta vifaa tiba huduma zianze kutolewa.


Aidha amewataka wananchi wa kata ya Rualuke kuchagua mafiga matatu ya CCM ili mpango huo wa kimkakati na sera ya taifa iweze kutekelezwa kijijini hapo.


Aidha akiwa katika kitongoji cha Mbawa Mgombea ubunge huyo wa jimbo la kibiti pia ameahidi kuendeleza kufuatialia hatua za upandishaji wa hadhi ya kitongoji cha Mbawa katika kata ya Lualuke ili kiwe kijiji iwapo CCM itashinda na kupewa dhamana ya kuongoza.


Mpembenwe amesema kitongoji hicho kina kila sababu ya kuwa kijiji anachakua hiyo kero ili kwenda kuifanyia kazi mara baada ya uchaguzi mkuu ili zile huduma za msingi za kijiji zipatikane hapo hapo mbawa.

++++++

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages