Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Beatrice Dominic akizungumza wakati akizindua Kamati za Afya za Kituo cha afya cha Sinza na Zahanati ya Malamba Mawili, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Lapaz, katika Manispaa hiyo jana. Picha: Bashir Nkoromo
Na Bashir Nkoromo, Ubungo
Kamati za Afya katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, zimetakiwa kuhamasisha wananchi katika makundi mbalimbali ya kijamii kujiunga na huduma ya Bima ya Afya ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic wakati akizindua Kamati za Afya za Kituo cha Afya Sinza na Zahanati Malamba Mawili, katika hafla iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Lapaz, uliopo uliopo Luguruni katika Manispaa hiyo, na kuongeza kuwa pamoja na kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya, pia Kamati hizo zinatakiwa zihakikishe zinashirikisha wadau wa maendeleo katika kuboresha afya ya jamii.
Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa pia na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dk.Peter Nsanya, Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Manispaa ya Ubungo Israel Sostheness na Wataalam kutoka katika Manispaa hiyo Kamati zilielekezwa majukumu yao ambayo ni kusimamia vituo kwa shughuli za kila siku, kusimamia maboresho ili wanachi wapate huduma bora za Afya ,matumizi ya dawa, kushiriki katika mipango ya kituo kila mwaka, Wajumbe hao pia wamefundishwa juu ya ukaguzi wa dawa vituoni(drug audit).
Akizungumza na Kamati zote za Afya Manispaa ya Ubungo kutoka zahanati,Vituo vya Afya na Hospitali Mkurugenzi aliwataka kufanya ukaguzi wa dawa kwenye vituo na kuwataka huduma za Bima ya Afya ya Jamii (iCHF) ianze na wao pia waihamasishe kujiunga na huduma hiyo jamii inayowazunguka, kisha akawapongeza wataalam wote ambao wapo kwenye vituo kwa kufanya kazi vizuri na kutoa huduma nzuri kama ilivyo kwenye Kituo cha Afya cha Sinza, Kimara na Mbezi.
"Niwaase wajumbe mkapate huduma katika zahanati na vituo vya afya vilivyopo katika Manispaa ya Ubungo ili kuongeza mapato". aliongeza Mkurugenzi
Vilevile aliwakabidhi miongozo wajumbe wa Kamati ya Afya Zahanati ya Malamba Mawili na Wajumbe wa kamati ya Afya Hospitali ya Sinza. Natamka rasmi Kamati ya Sinza na Malamba mawili imezinduliwa rasmi leo tarehe 12/9/2020
Aidha Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dk.Peter Nsanya aliwataka wajumbe kuwa mawakala wazuri wa kushawishi wananchi wa wilaya ya Ubungo kujiunga na bima ya Afya ya Jamii (ICHF) ili kupata huduma za afya kwa gharama nafuu.
"ICHF ni bima inayomsaidia mwananchi yoyote wa hali ya chini kupata huduma ya matibabu kwa gharama ya Tsh40,000 kwa mtu mmoja na 150,000/=kwa familia ya watu sita baba, mama na tegemezi wake wanne kwa mwaka mzima" aliongeza Mganga Mkuu.
Sambamba na hayo Mganga Mkuu aliendelea kuwakumbusha wajumbe kuwa ni muhimu wakatambua majukumu yao na kuzingatia misingi ya kazi zao.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Manispaa ya Ubungo Sostenes Israel aliwashukuru wajumbe wa kamati na kuwasihi kuzingatia majukumu yao na kuwapongeza kwa kazi nzuri ambazo zinafanyika.
Mkurugenzi aliwashukuru wajumbe kwa ujio wao na kuwapongeza kwa kujitokeza kwa wingi pia aliwaasa wakafanye kazi ipasavyo na kuwataka wakajitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi ili waweze kuchagua viongozi wao.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA HAYA HAPA👇👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇