LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 12, 2020

I&M BANK YAKUTANA NA WATEJA KWENYE CHAI YA ASUBUHI


Timu ya wafanyakazi wa I&M Bank ikiongozwa na mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Baseer Mohammed, wakuu wa idara mbalimbali, meneja wa matawi ya Dar es salaam pamoja na wateja katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M, Bw. Baseer Mohammed akiongea na wateja wakati wa kikao kifupi na wateja Golden Tulip siku ya Ijumaa 11 Septemba.
Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa Benki ya I&M,  Lilian Mtali akifafanua jambo wakati wa kikao cha wateja kilichofanyika ijumaa 11 septemba Hoteli ya Golden Tulip Masaki

.......................................................................

Benki ya I&M Tanzania leo 11 septemba 2020 imekutana na wateja wake katika Hotel ya Golden Tulip kama ilivyo ada ya Benki ya I&M Tanzania kukutana na wateja wake kwaajili ya kujadiliana mada mbalimbali zinazohusiana na huduma za kibenki, changamoto na njia za kuwapatia wateja wake suluhisho ili wafurahie huduma za benki yao. 

Akiongea kwenye kikao hicho, Baseer Mohammed Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo alisema, “Kwaniaba ya wafanyakazi wote wa Benki ya I&M napenda kuwashukuru wateja wetu wote mlioweza kuitikia wito na kuhudhuria kikao hiKi kifupi chenye mada zenye tija kwa maendeleao ya benki na wateja kwa ujumla.  Hiki kikao  kwaajili yenu hivyo msisite kuuliza maswali na kuchangia mada zitakazoleta maboresho makubwa kwenye huduma zetu.

Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja, Lilian Mtali pia aliongezea kwa kusema, “hiki kikao ni muhimu sana kwetu kwani tunategemea sana mrejesho wenu kuhusiana na huduma zetu na wapi tuboreshe ili kuhakikisha tunawapa huduma bora sana. Tunashukuru sana kwa mawazo yenu, maoni kuhusu maboresho pia pongezi mlizotupa tunawaahidi tutafanya Zaidi ili kuhakikisha I&M ni benki pekee ambayo mtakua mkiifikiria mtakapohitaji huduma bora za kibenki.

Wateja pia hawakua mstari wa nyuma kwani walifurahia sana ukaribu ambao benki hiyo umeweka kukutana na wateja wao na kuhakikisha wanapata huduma bora Zaidi na za kisasa za kibenki. Wameipongeza  benki ya I&M kwa huduma bora, uharaka katika kujibu changamoto za wateja, pia mifumo ya kidijitali kuhakikisha wateja wanapata huduma saa 24 kupitia iClick, na huduma za kibenki kwa njia ya simu *150*32#.

Mbali na matawi yaliopo Dar es salaam Nyerere, Maktaba, Tawi kuu, Kariakoo na Oysterbay, benki ya I&M pia ipo Moshi, Arusha na Mwanza na muda si mrefu inaanzisha huduma za wakala maeneo mbalimbali na mikoa mbalimbali ili kufikisha huduma kwa haraka.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages