Dk. Mabula akicheza wimbo wakati wa kampeni za CCM katika Kata ya Mecco
Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula,amesema yale atakayo ahidi atahakikisha anayatekeleza hivyo wananchi wakiamini chama hicho na kukipa kura za ushindi katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Alizungumza hayo kwenye mkutano wake wa kampeni wa kuomba kura kwa wananchi uliofanyika Mecco Kaskazini Kata ya Mecco,ambapo Dkt.Angeline amesema atahakisha ahadi zinakwenda kutekelezwa maana hapendi arudi tena hapo kipindi kingine halfu aanze kuulizwa kuwa alisema hili na hili lakini ujatimiza pia kauli mbiu ya awamu ya tano ni tumeahadi na tumetekeleza.
"Naomba niseme tunakwenda kufanya nini,nataka kuwahakikishia tu katika mwaka huu wa fedha tunaoendelea nao tayari zimetengwa milioni 151 ambazo zinakwenda kurekebisha baadhi ya miundombinu katika Kata hii ya Mecco kati ya hizo milioni 47 kwa ajili ya barabara ya Mecco-Kangae kwenda Makaburini kama hiyo haitoshi barabara ya Nyabulekerwa nayo ni mbovu kuna milioni 25 zimetengwa na zinakwenda kuanza kufanya kazi,"na kuongeza kuwa
"Tunayo barabara ya Gedeli shuleni kwenda Kangae nayo imetengewa milioni 28 pia daraja letu la Nundu kwenda kanisa la Wasabato lilikua lianze kutengeneza kabla ya mwaka wa fedha ule kuisha lakini lilichelewa kuanza kutengeneza nawahakikishia linakwenda kutengenezwa na kuondokana na adha iliopo katika eneo hili na barabara nyingine ambazo hazihitaji marekebisho makubwa yatakuwa yanarekebishwa kulingana na uhitaji" amesema Dkt.Angeline.
Amesema,zimetengwa milioni 20 kwa ajili kujenga madarasa shule ya msingi Nyabulekerwa na Nundu,hiyo yote ni kuhakikisha miundombinu inaboreshwa hawahitaji watoto wanaofeli na kuishia darasa la saba na hawawezi kwenda mbele kwa sababu mazingira waliokuwa nayo hayakuwa mazuri.
Kutokana na kuboresha miundombinu ya elimu katika shule za msingi na sekondari ndio sababu ya halmashauri ya Ilemela kufanya vizuri kwani hata zilizokuwa zinafanya vibaya walipeleka vitabu vya kujifunzi mfano shule ya sekondari Kilimani iliokuwa inashika nafasi ya 22 kati ya 24 ila sasa inashika nafasi ya pili hivyo wakiboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia matokeo chanya yanaonekana.
"Serikali ya Dkt.Magufuli imeona mwanafunzi akimaliza chuo nafasi za kazi zikitoka lazima awe na uzoefu wa miaka mitano sasa anaitoa wapi na yeye anakuwa ndio kamaliza chuo,Serikali ya CCM sasa inasema mwanafunzi akimaliza chuo watakwenda internship(mafunzo kwa vitendo),mwaka mmoja na zaidi ili waweze kupata uzoefu na kazi zinapotokea wasiulizwe juu ya suala hilo na utaratibu unaandaliwa,"amesema Dkt.Angeline.
Meneja Kampeni wa CCM Jimbo hilo Kazungu Idebe, amesema wanayosababu ya milioni 100 ya kumuamini Rais Magufuli na wagombea wa CCM kwani ameimarisha miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Jimbo hilo kwani wameshuhudia barabara,vivuko,meli,uwanja wa ndege,elimu bure,maji na umeme,aliwaomba wananchi kuchagua mafiga matatu ikiwemo Rais,Mbunge na Diwani kwa ajili ya maendeleo ya wanamecco na Jimbo zima.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Aziza Isimbula, amesema mwaka 2015 walitoa ahadi mbalimbali ambapo wamefanikiwa kuitekeleza hivyo wanaomba ridhaa kwa mara nyingine ili waweze kutekeleza yale yalio kwenye ilani ambayo imebeba matarajio na matamanio ya wananchi pia chama hicho kiba Mipango na dira ya kuwatumikia na kuwaletea wananchi maendeleo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇