LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 14, 2020

DK KABATI: WANAWAKE TUTAKIMBIA MCHAKA MCHAKA KILA JIMBO KUZISAKA KURA ZA DK MAGUFULI+VIDEO


 MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ritta Kabati amesema Wanawake wa Mkoa huo watakimbia mchaka mchaka kila jimbo kuzisaka kura Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli, wabunge na madiwani wa chama hicho.

Dk Kabati ambaye  kipindi kilichopita alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu, aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika Jimbo la Mufindi Kusini.

Mbunge huyo mpenda maendeleo kiasi cha kutunukiwa heshima ya Udaktari pia waliokuwa wabunge wenzie, walimchagua kuwa Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa huo, alisema wana kila haki ya kuipigia kura CCM, kwani maendeleo ya wazi yaliyoletwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli, yanaonekana.

Ili nisimalize uhondo msikilize Dk. Kabati anavyopiga kampeni kwa staili ya aina yake.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages