Mbunge Mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa kupitia CCM, Dk. Ritta Kabati leo amewaongoza wanawake katika maandamano ya kwenda kuwatembelea wafungwa gerezani na Hospitali kuwafariji wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kutafuta kura za ushindi kwa wagombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.
Katika maandamano hayo, Dk Kabati pamoja na wanawake wengine aliambatana pia na viongozi wa CCM wa mkoa huo, akiwemo Mgombea Ubunge wa Iringa Mjini kupitia CCM, Jesca Msambatavangu na wagombea udiwani.
Ili nisimalize uhondo nawaomba muendelee kutazama video hii iliyosheheni tukio hilo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇