Na Samirah Yusuph
Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Simiyu limeeza kuwa shughuli za ujenzi wa makazi ya kuishi bila mpangilio mzuri unakwamisha utendaji kazi wake.
Changamoto hiyo imekuwa ikiwafanya askari wa kupambana na Moto, kushindwa kufika kwa urahisi katika eneo linalokusudiwa kutokana na mitaa mingi hasa katika maeneo ya mijini kutokuwa na mpangilio mzuri wa ujenzi.
Akiitaja changamoto hiyo kuwa Ni moja ya sababu ya wao kupewa lawama nyingi yatokeapo majanga ya moto, akiwa katika viwanja vya naenane Nyakabindi Wilayani Bariadi.
Kamishna wa utawala na fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Sultan Semwanza alisema, licha ya kuwa wamefanya mwasiliano na mamlaka hisika Bado utatuzi was changamoto hiyo Ni mgumu.
"Tunamagari mengi na ya kisasa pamoja na vifaa vya kuzima Moto na uokozi lakini changamoto Ni tunapo fika huko mtaani Shida inakuwa Ni kutafuta wapi gari lipite ili huduma ipatikane," alieleza
Alisema kuwa wamejipambanua kutoa huduma kwa wateja wenye uhitaji, na kuwataka wananchi watoe taarifa mapema waonapo majanga ya moto ili jeshi Hilo liweze kufanya kazi yake kwa usahihi.
"Sisi kazi yetu Ni kuhudumia wananchi hivyo tunahitaji ushirikiano wao lakini pia wanafurusa kupitia sisi wakijifunza namna ya kukabiliana na majanga ya moto wa awali wafikapo katika maonyesho haya" aliongeza.
Akionyesha namna ya kutumia vifaa vya kuzima Moto wa awali station sagent katika Banda la nane nane Nyakabindi Wilayani Bariadi Mohamed Mkesa alisema, Ni wajibu wa Kila mmoja kuelewa namna ya kukabiliana na Moto wa awali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇