Kamishina wa Oparasheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Liberatus Materu Sabas amesema Jeshi hilo linafanya mafunzo ya kujiimalisha kwa kuwakabili waalifu nchini hasa kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi Mkuu.
Amesema hayo mjini kibaha wakati akifunga Mafunzo ya Utayari kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ambapo Askari 119 wamehitimu Mafunzo hayo ya mwezi mmoja, Sabas amesema kwa mafunzo wanajiimalisha na kujiweka sawa kiakili na kiafya kwaajili ya kukabiliana na wasiotaka kutii sheria bila shuruti.
Amesema yeyote atakayefanya ndivyo sivyo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwani wao ndio wasimamizi wa sheria nchini na amani ya nchi ikiwa ni pamoja mazoezi ya kawaida ya jeshi hilo.
Amesema Mafunzo ya Utayari kwa Jeshi la Polisi yameanza tangu mwaka jana na ni endelevu kwa askari hao hadi kipindi cha Uchaguzi Mkuu ujao ambapo tayali yamekwishafanyika katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Iringa na mkoa wa kipolisi Rufiji na Mtwara, Lindi na Ruvuma .
Aidha Sabas ameahidi nchi kuendelea kuwa salama kipindi chote hadi kukamilika kwa uchaguzi Mkuu chini ya usimamizi wa Jemedari Mkuu na Amili Jeshi Mkuu Mheshimiwa Docta John Pombe Magufuli kwani usalama unaimalishwa na vyombo vyote vya usalama.
“Na tutahakikisha usalama unaendelea kuwepo nchini kwa ulinzi unaosimamiwa na vyombo vyote vya usalama nchini kote” alisema Sabas.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇